Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uratibu, Sera na Bunge), William Lukuvi.
Matukio ya uhalifu yameendelea kushika kasi nchini, baada ya majambazi kuwapora raia wa China mamilioni ya fedha mkoani Iringa katika jimbo la Ismani la Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uratibu, Sera na Bunge), William Lukuvi.
Walioporwa fedha hizo Sh. milioni 135 ni Meneja wa Fedha wa kampuni ya SIETCO inayojenga barabara ya Iringa- Dodoma, Zhao Yang (23) raia China wa wenzake wanne. Vitu vingine vilivyoporwa ni simu tano za mkononi na funguo za gari.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo juzi mchana katika mlima wa Nyang’oro uliopo kata ya Ismani.
Kamanda Mungi alisema kuwa raia hao wa China waliporwa fedha hizo wakiwa ndani ya gari yenye namba ya usajili T. 335 CMX aina ya Toyota Fortuna, wakati wakitoka kuzichukua katika benki ya CRDB iliyopo mjini hapa. Haikuweza kufahamika mara moja fedha hizo walizichukua kwa ajili ya shughuli gani.
Kamanda huyo alisema kuwa walizichukua fedha hizo bila kuwa na ulinzi wowote.
Kwa mujibu wa Mungi, baada ya kufika katika mlima huo, raia hao wa China walikuta lori kubwa limefunga njia na kulazimika kusimama ili kujua kinachoendelea.
Kamanda huyo alifafanua kuwa baada ya kusimama, lilijitokeza kundi la vijana watano wakiwa na bunduki na kuwaamuru wawapatie mfuko wenye fedha.
Alisema Wachina hao walitii amri hiyo, lakini majambazi walitumia nguvu na kuwanyang’anya funguo za gari pamoja na simu tano kisha kutoweka.
Alisema baada ya tukio hilo Polisi walifanya msako mkali kwa kushirikiana na wananchi na kufanikiwa kumkamata jambazi mmoja akiwa kwenye basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace eneo la kijiji cha Itono.
Hata hivyo, baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, wengine wanne walikimbilia kusikojulikana na kwamba Jeshi hilo linaendelea kuwasaka.
Katika hatua nyingine, Kamanda huyo, alisema jana alfajiri Polisi wakiwa katika msako huo, waliokota mabegi mawili, moja likiwa na Sh. milioni 80 na lingine likiwa na biscut na vitu vingine vya Kichina.
Alisema kuwa kabla ya kuokuta mabegi hayo, walirushiana risasi na majambazi yaliyokimbia awali.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment