Robert Manumba
Jeshi la Polisi Nchini limesema halina taarifa za kukamatwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec), Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, Aggrey Kalolo kwa tuhuma za ujangili.
Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Issaya Mungulu, akizungumza na NIPASHE jana kwa njia ya simu alisema hajapata taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo.
“Mimi sina taarifa za kukamatwa kwa mtu huyo unayeniambia na wala sijaletewa taarifa kutoka huko,” alisema.
Wakati Mngulu akisema hajapata taarifa zozote kuhusiana na kada huyo kutuhumiwa kwa ujangili.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Deusidedit Nsimeki, juzi alithibitisha Kalolo kukamatwa kuhusiana na tuhuma hizo.
Hata hivyo, Nsimeki juzi alikataa kueleza kwa undani juu ya tukio hilo kwa maelezo kuwa lipo kwenye kampeni maaalumu ya kitaifa.
Alisema mtuhumiwa alikamatwa siku kadhaa zilizopita na kuachiwa kwa dhamana. Pia juzi aliachiwa kwa dhamana baada ya mahojiano.
Nsimeki alisema yeye siyo msemaji kwa kuwa kampeni hiyo inashirikisha vyombo vingine vya dola, hivyo hawezi kulizungumzia tukio hilo zaidi mpaka hapo wakubwa watakapotoa ripoti ya jumla kuhusiana na matukio mbalimbali ya ujangili mkoani Ruvuma.
Naye DCI Manumba, juzi alipoulizwa kuhusiana na tukio la kada wa CCM kukamatwa, alisema hana taarifa zozote kwa kuwa yuko nje ya nchi na kumtaka mwandishi kuwasiliana na wahusika wengine.
Alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo, Kalolo alithibitisha kukamatwa na Jeshi la Polisi na kufafanua kwamba baada ya kupekuliwa nyumbani kwake hakukutwa na kitu chochote kinachoonyesha ushahidi juu ya tuhuma hizo.
Hivi karibuni wanyamapori, hususan tembo wamekuwa wakiuawa kwa kasi na kutishia sekta ya utalii chini.
Takwimu zinaonyesha kuwa takriban tembo 30 wanauawa kila siku katika hifadhi za taifa na katika mapori ya akiba.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment