ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 28, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WATOA POLE KWA MJANE NA FAMILIA YA BALOZI WA ISAAC SEPETU

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu  alipokwenda  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole. Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
Mama Salma Kikwete  akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam. . Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akimfariji mjane wa Balozi Isaac Sepetu, wakati yeye na mkewe Mama Salma Kikwete (picha ya chini) walipokwenda nyumbani kwa marehemu Sinza Mori jijini Dar es salaam  kutoa pole. Balozi Sepetu alifariki dunia jana asubuhi kutokana na kiharusi na kisukari. Kwa mujibu wa duru za kifamilia marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano Oktoba 30, 2013 huko Mbuzini, Zanzibar.
Mama Salma Kikwete akimfariji mjane wa Balozi Isaac Sepetu, wakati yeye na mmewe Rais Kikwete (picha ya juu) walipokwenda nyumbani kwa marehemu Sinza Mori jijini Dar es salaam  kutoa pole. Picha na Ikulu

No comments: