Advertisements

Wednesday, October 16, 2013

SHEREHE YA EID DMV YAFANA

Imam Hussein Ibrahim akiongoza swala kwenye sherehe y Eid iliyofanyika Jumanne Oct 15, 2013 DMV na kuhudhuriwa Watanzania wa DMV .
Waumini wa dini ya Kiislam wakiswali kwenye sherehe ya Eid iliyofanyika Wheaton, Maryland na kuhudhuriwa na Watanzania na marafiki zao waishio DMV na vitongoji wa jirani.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislam DMV (TAMCO) Bwn. Yusuf(kati) akiongea jambo kwenye sherehe ya Eid iliyofanyika Wheaton, Maryland Jumanne Oct 15, 2013 wengine kwenye picha ni Imam Hussein Ibrahim (kushoto) na mjumbe wa bodi ya udhamini ya TAMCO, Bwn. Seif Ameir
Kutoka kushoto ni Dkt. Hamza Mwamoyo, Jasmine Barnett, Rais wa Jumuiya DMV bwn. Idd Sandaly na Mganga Muhombolage wakiwa meza kuu.
Watanzania waliohudhuria sherehe ya Eid.
Aunt Asha na mumewe.
Moza kutoa New York akiwa kwenye sherehe hiyo ya Eid iliyofanyika DMV Jumanne Oct 15, 2013
Watanzania waliohudhuria sherehe hiyo.
Watanzania na marafiki zao wakiwa kwenye sherehe ya Eid
wakati wa chakula.
Click soma zaidi for more photos.

4 comments:

Anonymous said...

Najua sherehe ni sherehe, lakini kamwe haiwezekani kusiwe na tofauti kati ya sherehe za kidini na sherehe za kisecular.
Jamani ni hatari kuchanganya madawa, twende tukijiuliza uliza.
Kwa nini sherehe ya Eid ifanane na discotheque?
Kuna haja kufanya hivyo?
Au ndio kuishi mtoni?
Itaingia akilini endapo tukikubali kuacha utamaduni wetu upande mmoja tunapoamua kutenda matendo ya dini, otherwise tutakuwa tunajifurahisha sisi na kumuudhi Allah.
Tukumbuke kuwa Eid ni sherehe iliyopangwa na Allah, so sisi Waislamu tusiisherehekee kwa kuiga wasiofata matendo ya Kiislamu. Matokeo yake kizazi chetu kitakwenda kombo na sisi ndio tutasimamishwa kujibu kwa kuwa ndio sababu ya kupotoka kwa kizazi chetu.
Mwenyezi Mungu atusamehe.
Mdau, UK

Anonymous said...

Acha majungu wewe..hapo palikuna hotba na mawaidha ..eid ni sku ya kusherehekea sio maulidi wala hitma hiyo..wala sio siku ya ibada ni siku ya kusherehekea, wa2 wamekuja na kuvaa kiheshma na kulikua na michezo ya watoto sasa wewe unaeenda disco na.kanzu wacha majungu na uko hapa hapa dc..ndio nyinyi mnaosoma hitma siku ya eid..wacha maneno mengi ya kijinga kama hujui dini soma na jifunze...uislamu ni dini rahisi ya amani na upendo watu kama nyie ndio mnaipa dini jina baya .. Mwenyezi pia hapendi fitna na ubadhirifu.

Anonymous said...

Wewe mdau wa kwanza tushakujua!! Inaelekea wewe hujatembea hapa duniani NENDA DUBAI , Muscat, Abu Dhabi, DOHA UKAONE jinsi misikiti inavyopambwa na Mataa na Madudu kibao ya kumeremeta. Kama upo UK ALIYEKUPA HABARI KUWA KULIKUW na disco AU sijui upukupuku gani uliosema ni nani? WATU WALIVAA KAMA WAISLAMU WOWOTE DUNIANI UMEONA PICHA YA MTU ALIYEVAA KAMA YUPO DISCO???of course kaswida zilikuwepo zikipigwa hivi wewe hili ndo Discotheque Kama unavyodai AU WATU hamuishi kashfa hata kwenye Jambo la Imani bado mtatoa kashfa. Kama hukuweza Kuja kwa sababu zako binafsi keep it to yourself!! QURAN ILISOMWA na watoto na WATU wazima. Dua na mambo ya Fardhi yaliongelewa. Hongereni Kina dada mliopamba na kupika next year tunahamia MARRIOTT NDO USEME ZAIDI. WAISLAMU WENZANGU TULIOSTAARABIKA TUSONGE MBELE. Inshaalah na Madras ya KITANZANIA TUTAIFUNGUA.

Anonymous said...

Tena huyu aliyeandika ni wa hapa hapa DC tunawajua wooote wenye majungu hapa TAMCO! TUNATAKA AMANI NA UPENDO KAMA DINI YETU INAVYOAGIZA. NDO WALEWALE WANA VAA MASHUNGI YA KIFAHARI KUJIONYESHA TUU MWEZI WA RAMADHANI NA SIKU ZA EID, MWEZI WA TOBA UKIISHA UTAWAKUTA NA VIMINI WAMEKAA BAA. UISLAMU NA POMBE HAUENDI KAMA WEWE KWELI UNAIJUA DINI BASI MATENDO YAKO YAENDE SAWA NA VILE UISLAMU UNAVYOAGIZA IN 365 DAYS IN A YEAR YOU BETTER BEHAVE AS SUCH. TAKASENI NDIMI ZENU ACHENI MATUSI KWENYE MITANDAO NA MAGOMVI YASIYOKWISHA NA YASIYO NA BASE. KILA BINAADAMU KAUMBWA NA UZURI WAKE HAKUNA ALIYE MZURI AU BORA KULIKO MWINGINE HIZI SHUGHULI ZA KIDINI NI ZA KWETU SOTE. MATANGAZO YALITUMWA KUHUSU HII SHEREHE NA KAMA UNGETAKA KUCHANGIA MAWAZO YA KUPAMBA AU KUPIKA IT WAS JUST A SIMPLE EMAIL UNGETUMA KWA WAISLAMU WENZAKO KUWAAMBIA JAMA MIMI NINTALETA MAPAMBO SO UKAE WATU WASHUGHULIKE NA KUTUMIA PESA ZAO HALAFU ETI WAJA DAI WEWE NI MDAU WA UK! BASI WEWE NI MTU FITNA KAMA FROM UK USHAPATA HABARI ZOOOTE ULIZOZISEMA NA UNATAKA KUHAMISHIA FITNA ZAKO HUKU MD UMEKOSEA. HAPA WAISLAMU TUMEIMARIKA NA TUNACOMMUNITY YENYE VIONGOZI MAHIRI. INSHALLAH TUTAKUOMBEA KWENYE DUA ZETU MWENYEZI MUNGU AKUONDOLEE YOTE YANAYOKUSIBU!