Msanii Nguli wa Uigizaji wa filamu Tanzania Steven Megele almaarufu Steve Nyerere akielezea ujio wa nguvu wa filamu yake mpya iitwayo Long Time ambayo imetengenezwa na Kampuni ya Proin Promotions wakati alipofanya mkutano na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari leo Katika Ofisi za Proin Promotions zilizopo Mtaa wa Ursino Jijini Dar.Filamu hiyo pia itasambazwa na kuuzwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited kupitia Mawakala wao Nchini Nzima kuanzia leo
Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Evans Stephen (wa Kwanza kulia) na Msanii Nguli wa Filamu Tanzania Steve Nyerere kwa pamoja wakionyesha ukurasa wa filamu mpya ya Proin Promotions iitwayo long Time mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Proin Promotions zilizopo Mtaa wa Ursino Jijini Dar Steve Nyerere akiongelea ujio wa Nguvu wa Filamu yake mpya iitwayo Long Time ambayo inaingia sokoni leo, Filamu ambayo imeigizwa kwa ustadi wa hali ya juu na kuwa na uhalisia wa maisha ya Mtanzania.
Meneja Masoko wa kampuni ya Proin Promotions Bw Evans Stephen akiongelea juu ya ujio wa nguvu wa filamu ya Long Time iliyoigizwa na Wasanii mahiri Steve Nyerere na Johari.Filamu hiyo imetengenezwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited na itasambazwa na kuuzwa na Mawakala Wa Proin Promotions Limited Nchini Nzima na itaanza kupatika leo katika Sehemu Mbalimbali za Tanzania.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano na Msanii wa Filamu Tanzania Steve Nyerere akiwa pamoja na Meneja masoko Wa Proin Promotions Bw Evans Stephen wakati wakiitambulisha filamu mpya kutoka Proin Promotions iitwayo Long Time
Mmoja wa waandishi wa Habari (katikati) akiuliza swali kwa mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Proin Promotions ambao ndio watengenezaji,wauzaji na wasambazaji wa Filamu yao Mpya iitwayo Long Time ambayo imeigizwa na Wasanii mahiri na nguli Steve Nyerere, Johari na wengine wengi .
Kampuni ya utengenezaji,uuzaji na usambazi wa filamu za kitanzania Kutoka nchini Tanzania ya Proin Promotions leo imetambulisha rasmi filamu yake mpya iitwayo Long Time ambayo itapatikana kuanzia leo sokoni kwa gharama ya Shilingi Elfu tano tu za kitanzania
Filamu ya Long Time ni filamu ambayo imetengenezwa na kampuni mahiri ya Proin Promotions limited na kuigizwa na wasanii wakongwe na nguli wakiwemo Steve Nyerere, Blandina Chagula na wengine wengi.
Proin Promotions limited imejikita katika kubadilisha soko la filamu Tanzania na kuleta mapinduzi ya kweli katika tasnia ya filamu nchini,Na takribani nakala laki moja za Filamu ya Long Time zishaingia soko leo na kuuzwa.
Long Time ni filamu ambayo inafundisha na kuburudisha na pia inayoelezea Uhalisia wa maisha ya Mtanzania.
No comments:
Post a Comment