Hawa ni vijana wa kitanzania 11 ambao walikamatwa na jeshi la polisi Mtwara baada ya kupata taarifa kwamba walikua wakifanya mazoezi ya kivita kwa kutumia CD za Al Qaeda na Al Shabaab ambapo walikamatwa na hizo CD pamoja na silaha mbalimbali kama ushahidi...
Taarifa ya jeshi la Polisi leo imesema kuwa , vijana hawa walipelekwa Mahakamani na watarudishwa tena tarehe 4 November 2013.
Juu na chini vijana hao wakishuka kwenye gari la polisi lililowaleta mahakamani leo.
Nje ya mahakama kukiwa na ulinzi mkali.
Mmoja wavijana akielekezwa mlango wa mahakama.
Juu na chini vijana 11 wakiwa mahakamani.
9 comments:
Sasa Police wawafinye mpaka what oboe Siri zoote! Nani anawaruma? Pesa wanatoa wapiti za kufanikisha hayo mazoezi maana tumeona wana DVD zilizotengenezwa vizuri tu! Na chakula wanapewa na nani maana imesemekana wanashinda wakijifunza hayo mafunzo sasa bila kufanya kazi wanakula waapi? Mnunuzi wa chakula chao Ni nani? Police msiwaachie endaikawa mtandao wao in mkubwa sana!
kisingizizo hichi unadhani watu bado wajinga mnajua wakina nani waovu mbona hamuwakamati mnapigania vita chini ya mwavuli wa kidini na ugaidi wakati mnajua ukweli ni wa kinani wanao haribu nchi.
mungu atawasaidia wote wanaoshitumiwa tanzania yetu ni ya kuwababikizia kesi waislamu kila leo unadhani nani hajui hili mungu mkubwa lakini atalipa hapa hapa duniani kesho hisabu amin
Hakuna lolote la maana na wala si magaidi hao zaidi ya danganya toto tu maana magaidi wa ukweli huwa hawana muda wa kukaa maporini... Kuna yule mTZ aliyekuwa Al-Queada mbona hakuwa porini na alifanya majanga haswaa. Kwa kifupi hizi ni porojo tu
serekali yetu yakiwehu leokiongozi akiamka anasema atakalo ilimradi aonekane nayeye anafanya kazi asifiwe na rais. gaidi gani shati limechanika namna hiyo chini anandara ya mgogo, walikuwa wajalibu kutafuta madini hao wanawasingizia magaid. gaidi gani anajifunza ugaidi nakisu cha kuchinjia kuku,kama mnaona kenya wana faidi watakujatu nyinyi endeleeni kuwaombea
Hakuna cha ugaidi wala nini sijui. Magaidi watakuwa hao!!?? PoliceCCM kila siku ni kuja na agenda za ajabu ajabu. Vijana wamechanganyikiwa kwa maisha kuwa magumu, huku rasilimali zao zinasubiri kuchukuliwa na wafungwa kutoka CHINA (si wameonekana Addis Ababa safarini Mtwara) badala ya kuwanufaisha wana-Mtwara!!
Mbona shitaka la ugaidi limeshafutwa na haijulikani wamesukumiziwa lipi ?
Huu umwema naona unatafutwa kwa nguvu zote, mbona hatuambiwi kuhusu CD za akina Rambo, schwarzenegger? vijana walikua na mapanga,majembe, mafyekeo lakini hatuambiwi kuhusiana na hilo.
Kafara hao kuna big picture nyuma ya pazia.
We mjinga kweli kwani mjaidina wanavaa suit mbona wanashinda milimani wanalala kwenye mapango
Post a Comment