Mashabiki wa Mbeya City wakiishangilia Mbeya City katika moja ya mchezo wao wa Ligi kuu Vodacom Bara.
Uongozi wa Klabu ya Mbeya City umesema unataka mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC iliyopangwa kufanyika Alhamisi wiki hii katika Uwanja wa Azam Complex (Chamazi), isogezwe mbele huku ukifanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Azam inaongoza katika msimamo wa ligi kutokana wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa, lakini kwa upande wa pointi ina 26 sawa na Mbeya City zikifuatiwa na Yanga (25) na Simba (21).
Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana, Katibu Mkuu wa Mbeya City, Henry Kimbe, alisema watawasilisha barua yao kwa Shirikisho la Soka nchini (TFF) ili kuomba kufanyika kwa mabadiliko hayo hasa kutokana mazingira halisi yanayozunguka mchezo huo.
Kimbe alisema wanaamini mchezo huo utavuta mashabiki wengi wa soka wa jijini Dar es Salaam na kwamba kama utachezwa Alhamisi, utawafanya mashabiki wengine kwenda Uwanja wa Taifa kuiangalia Yanga itakayokuwa inacheza na JKT Oljoro siku hiyo.
"Kwetu tumefikiria na kuona kuna ulazima wa mabadiliko, tunataka kuwapa burudani mashabiki wetu, ikichezwa Chamazi itakuwa tatizo. Tunataka watu wa mjini watuone," alisema katibu huyo.
Aliongeza kuwa, kama TFF hawatakubali kufanya mabadiliko hayo, wanatarajia kutua jijini Alhamisi mchana kwa ndege tayari kuikabili Azam siku hiyo.
Naye msemaji wa Azam, Jaffer Iddi, alisema jana kuwa, wao hawako tayari kuona mechi hiyo ikisogezwa mbele ama kubadilishwa uwanja kama ilivyopangwa awali.
"Sisi hatuko tayari kwa mabadiliko yoyote, kama wanaona uwanja ni mdogo, basi waombe mechi yao ya marudiano ichezwe Taifa badala ya sisi (Azam) kwenda Mbeya, " alisema Iddi.
Kwa upande wa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura, alisema jana kuwa, tayari wameliona hilo na watawasiliana na viongozi wa klabu hizo mbili kwa ajili ya kupata mawazo yao.
Wambura alisema yatakayoamuliwa na viongozi wa klabu hizo ndiyo watakayofuata na si vinginevyo.
Azam yenye tiketi ya kuiwakilisha nchi mwakani katika mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika na Mbeya City iliyopanda Ligi Kuu Bara msimu huu, ndizo timu pekee ambazo zimeweka rekodi katika mzunguko wa kwanza kwa kutofungwa baada ya kushuka dimbani mara 12.
Uwanja huo wa Azam Complex ambao ni wa nyumbani kwa Azam, unauwezo wa kuingiza mashabiki 7,000 tu.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment