ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 25, 2013

MTAZAMO WA PICHA HIZI UNAWEZA KUKUPATIA MAJIBU YA KUKANGANYA UKAFIRIA KUWA KUNAKITU ZAIDI KINAENDELEA

PICHA za aliyekuwa mke wa marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Wastara Juma akiwa na mwigizaji Bondi bin Salim ‘Bond’ zimezua utata ambao unakazia ukweli wa taarifa ya kuwa wawili hao ni wapenzi.
Kikizungumza na Ijumaa Wikienda chanzo chetu kilicho makini, kilisema kinawashangaa sana Wastara na mwenzi wake huyo kuukana upenzi wao kila kukicha wakati picha zinajieleza.

“Wastara amekuwa akimkana Bond kuwa si mpenzi wake ila ni kaka yake sasa hebu tazama picha zao mpya, hata mtoto mdogo humdanganyi kitu,” kilisema chanzo hicho huku wawili hao wakiendelea kukanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi. 

-GPL

1 comment:

Anonymous said...

maskini sajuki mungu amlaze pema peponi allah ma amin dunia ya leo kweli hakuna mapenzi