ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 14, 2013

MUME AU MKE KULOCK SIMU NA KUWEKA PASSWORD NI SAWA AU?, JAMAA ANAHISI ANAIBIWA HUYU MKE KWA KUPASSWORD SIMU YAKE

''Nampenda sana mke wangu, ni miezi sita tu toka tufunge ndoa!!!
sitaki kumuudhi wala kumkera kwa lolote, namtimizia kila kitu ili mradi tu asipate vishawishi vya kutoka nje ya ndoa!
toka tuanze mahusiano yetu ya kindoa, mke wangu alikuwa msikivu sana kwangu, kila ninalo mwambia amekuwa 

akinisikiliza! ilifikia kipindi ikawa ni utamaduni wetu kuwa tuna share mpaka simu zetu! yeye akiwa anatumia yangu mi

natumia yake! wiki chache hivi zilizopita, nimeshangazwa sana na hiki kitendo nilichokuta kwenye simu ya mke wangu, simu yake imefungwa kwa namba maalum anazozijua yeye mwenyewe!! nilipojaribu kuhoji juu ya hilo, akanijibu kwa ukali, ''kwani wewe unataka nini, simu si yangu, na wewe una yako.. funga na wewe yako''!

niliamua kukaa kimya ili nisizue mengine! mke wangu amekuwa ni mtu wa kupokea simu za ajabu ajabu na kutumiwa meseji kila mara, kila ninapohoji, yeye anasema kwa ukali kwamba wivu, namwaibisha kwa mashoga zake... eti tuko mjini hapa!!!

mwenzenu nimechanganyikiwa!!! nahisi kunyang'anywa tunda langu''......

2 comments:

Anonymous said...

kwa kweli kama huna ufichacho why password,yawazekana ana marafiki wa mitandaoni wanaiita cyber sex.kwa kweli hii bado ni kuwa na mausiano tu na mtu kwani mwishoni watu wanaishia kukutana au kuzua matatizo makubwa ikiwa huyo mshiriki wa cyber sex akimpenda na kutafuta njia za kukuangamiza na kumshauri wawe na mausiano ya kweli,kaka kuwa makini kuna kitu kinaendelea, kama hamna siri kwanini awe na wasiwasi ukishika simu. ndugu zangu mapenzi ya kweli yako wapi hii pia ni moja ya uzizi kwani unashare mapenzi na mtu mwingine.ukiwa kwenye ndoayayoishia kuumizana roho na kupunguza uaminifu.where is trust in relationship if u trust things like this happen.

Anonymous said...

Hakuna watu waongo kama mademu wa bongo aisee. Hawa viumbe ni waongo wa kutupwa kabisa. Anza kujiandaa chief hapo juu maana ukimwi unaua na bongo watu wako kwenye circle demu ana mabwana kumi. shaking my head. Taifa linaangamia. Huyo wife mpige chini fasta kabla malaria hiyo haijapanda kichwani.

MBEBA BOX MAARUFU DA WHITE HOUSE
1600 PENNYSLVANIA AVENUE