Wakati Yanga kesho ikishuka Uwanja wa Taifa kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kucheza na JKT Oljoro, inahofia Azam FC inaweza kuwapokonya ubingwa huo msimu huu.
Azam inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 26 kileleni sawa na Mbeya City inayozidiwa kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa huku Yanga yenye pointi 25 ikishika nafasi ya tatu baada ya timu zote kushuka dimbani mara 12.
Akizungumza na NIPASHE jana mara baada ya mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika katika Uwanja wa Kijitonyama badala ya ule wa Loyola kutokana na kujaa maji, Kocha Msaidizi wa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, Fredy Felix Minziro, alisema timu wanayoihofia katika mbio za ubingwa ni Azam tu.
Minziro aliwatoa watani wao wa jadi, Simba kwa kudai kuwa ni wasindikizaji katika mbio hizo msimu huu, huku akifafanua kuwa kasi ya Mbeya City ni nguvu ya soda.
Alisema, Yanga haina wasi wasi wowote na matokeo ya mechi ya kesho kati ya Azam na Mbeya City ambayo itachezwa Uwanja wa Chamazi, lakini hofu yao ni namna ya kuipiku Azam ambayo imeonyesha ubora huku ikiongoza ligi hiyo.
"Hatuna wasi wasi na Simba wala Mbeya City, kwa sababu wote ni nguvu ya soda, Azam ndio wapinzani kwenye ubingwa," alisema Minziro.
Alisema, kutokana na hilo, kikosi chao kitaingia kambini katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Jangwani jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujiandaa vema na mchezo wa kesho dhidi ya JKT Oljoro.
Alisema kwa sasa timu hiyo imehamishia mazoezi katika Uwanja wa Kijitonyama kwa muda kutokana na mvua zilizonyesha jana maeneo mablimbali ya jijini Dar es Salaam ambazo zilisababisha Uwanja wa Loyola kujaa maji.
Akizungumzia mechi hiyo, Minziro alisema ni muhimu kwao kushinda ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wao.
Alisema wachezaji wote wako fiti na wanaendelea na mazoezi, isipokuwa majeruhi Nizar Khalifan, Athuman Idd 'Chuji', Salum Telela, Juma Abdul na David Luende.
"Nizar, Chuji, Telela na Mbuyu Twite wameanza mazoezi mepesi, ninaimani wataendelea vizuri kwa ajili ya kujiandaa na mechi ijayo," alisema Minziro. Licha ya Minziro kuipuuza Mbeya City, timu hiyo na Azam ndizo timu pekee ambazo hazijapoteza mechi yoyote baada ya kushuka dimbani mara 12 na kujikusanyia pointi 26.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment