ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 6, 2013

CHAMPIONI, HANSPOPE WAMSAIDIA MATIBABU KOCHA SIMBA

Mwandishi wa gazeti la Championi, Khatim Naheka (kushoto), akimkabidhi kocha wa makipa wa Simba, James Kisaka kiasi cha Sh 350,000 zilizotolewa na gazeti la Championi pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hanspope ili kusaidia matibabu. Kulia ni Mhariri Kiongozi wa gazeti hilo, Saleh Ally akishuhudia tukio hilo nyumbani kwa Kisaka.
...Mwandishi wa gazeti la Championi, Khatim Naheka (kushoto), akimpa mkono kocha wa makipa wa Simba, James Kisaka, Kulia ni Mhariri Kiongozi wa gazeti la Championi, Saleh Ally akishuhudia tukio hilo nyumbani kwa Kisaka.

Kisaka, kipa wa zamani wa Volcano ya Kenya amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa unaosababisha mwili wake kukosa nguvu upande mmoja ingawa mwenyewe amesema si kupooza kama ilivyoelezwa awali.

Amekuwa akiendelea na matibabu, hata hivyo, Kisaka alilalama kushindwa kuhimili gharama kubwa ya matibabu hivyo kuwaomba wadau wajitokeze kumsaidia.

Championi likachukua nafasi ya kuomba wadau wajitokeze kumsaidia lakini uamuzi ukawa ni kuanza kuwa mfano kwa kutoa angalau kiasi cha fedha ili kuwahamasisha wadau kumsaidia Kisaka ambaye hata kutembea, analazimika kusaidiwa.

PICHA NA WILBERT MOLANDI.

No comments: