Mbwana Samatta akipambana na mabeki wa KenyaTANZANIA Bara ‘Kilimanjaro Stars’, imefungwa 1-0 na Kenya ‘Harambee Stars’ katika Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Uwanja wa Nyayo, Nairobi, usiku huu ikisindikizwa na mvua.
Kwa matokeo hayo, sasa Stars itamenyana na Zambia katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu keshokutwa mchana Uwanja wa Nyayo tena, wakati Kenya itamenyana na Sudan katika Fainali jioni yake.

No comments:
Post a Comment