ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 22, 2013

Unyama zaidi wabainika Operesheni Tokomeza

Hii ndio moja ya unyama uliofanyika kwenye Operation Tokomeza Ujangili iliyosimamiwa na washiriki toka Wizara 4 za mawaziri waliondolewa juzi bungeni.

Dar es Salaam. Unyama zaidi umebainika katika taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuhusu Operesheni Tokomeza Ujangili baada ya kubainika kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, Francis Miti, kukiri kujihifadhi kwenye hoteli moja nje ya wilaya yake.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli akisoma ripoti hiyo bungeni juzi alisema Operesheni Tokomeza Ujangili, ulisababisha hofu miongoni mwa wananchi na viongozi na baadhi yao kuyakimbia makazi. Lembeli alisema watuhumiwa, walikamatwa, walipekuliwa na  kudhalilishwa na baadhi kutojulikana walipo.
“Baadhi ya wananchi wakiwemo viongozi, madiwani na wenyeviti wa vijiji na vitongoji na watumishi wa Serikali, walikamatwa na kudhalilishwa mbele ya wananchi wanaowaongoza,” alisema Lembeli
Aliongeza; “Watuhumiwa waliokamatwa walidai kudhalilishwa mbele ya wanafamilia kwa kupewa adhabu wakiwa uchi na wanawake kushikwa sehemu za siri bila ridhaa yao.”
Lembeli alitoa mfano kuwa Ali Nyenge (38) wa Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga alidai kuvuliwa nguo, kumwagiwa maji yaliyochanganywa na chumvi na kuchapwa viboko huku mwanawe wa kiume (11) akishuhudia huku akilazimishwa kuchora picha ya Chatu kwa kutumia wembe kwenye paja lake.
Alisema mwanamke mmoja wa  Babati (jina tunalo) alidai kuvuliwa nguo na kulazimishwa kufanya mapenzi na wakwe zake, pia kuingizwa chupa sehemu zake za siri.
Aidha, baadhi ya wanawake walidai kubakwa na kulawitiwa huku wilayani Ulanga, mwanamke mmoja alidai kubakwa na Askari wawili wa Operesheni Tokomeza Ujangili mida ya usiku.
MWANANCHI

6 comments:

Anonymous said...

Mulipotuulia ndugu zetu na wazee wetu Pemba. Haikuwauma. Walipouliwa na kudhalilishwa ndugu zenu ndio munajifanya inauma. Justice has no boundaries. Arrest Mkapa too.

Anonymous said...

Kwa mara ya kwanza leo kusoma habari hii, na inaonekana ni matukio ambayo yana taarifa nyingi ambazo sijui ukamilifu wake, ila nimestushwa sana na taarifa hizi. Kwanza nilifikiri tukio hili na picha hii ni sehemu ya nchi ya somalia. Jamani naomba mtupe taarifa kamili juu ya hili kwani ni jambo ambalo linatisha vibaya sana. Is my hope sio Tanzania mambo haya yanapoendelea.

Kama ni tanzania, tutakuwa tumefika mahala pabaya sana, na pa kutisha.

Unknown said...

Inasikitisha sana kwa nchi kama Tanzania tunaosifika kama kisiwa cha amani, halafu amani yenyewe inaishia katika maandishi tu hakuna uhalisia wa amani kama inavyoandikwa. Tufike mahali tuseme utesaji umetosha, wakoloni walitesa babu zetu hadi leo athari zinaonekana tunaanza kutesana sisi kwasisi nchi inakwenda wapi?
Na tatizo ni kwamba mamlaka zinazohusika hazichukui hatua pindi aliyeteswa anapokwenda kulalamika. Hebu jaribuni kufanya upelelezi katika maeneo yanayozungukwa na mbuga za wanyama mtaona ni jinsi gani watu wanaonewa. Anakuja mtu atatokako hakujulikani anazungumza na vijana na kuwapa chochote kisha wamuorodheshee watu wanao husika na ujangili, baada ya hapo wanakuja siku inayofuata tena usiku wanakamata watu na kuwatesa bila kujali majina hayo yana ukweli kiasi gani. Hayo katika picha trela mwende katavi mkashuhudie makubwa mtakubali mkoloni katurithisha tabia mbaya.

Anonymous said...

Tumeshafikia pabaya siku nyingi bro. Nchi hsina mbele wala nyuma. Rushwa imefanya nchi nzima kuwa lawless country. Tanzania haina baba wala mama. We are at a point of no return.

Anonymous said...

Pinda should be voted out!, Where is the President of Tanzania??!!

Anonymous said...

kwa kweli huu ni aina ya unyama wa wananchi na haki za binadamu hazijazingatiwa, mawazili husika tiali washa wajibishwa bado askari kama watendaji wakuu wa matukio hayo.