
Hatari lakini salama. Huyu jamaa anajulikana kwa jina la Robert Buck, kwajina la utani au A.K.A ni Naked Cowboy akiwa Times Square New York City. Huwezi kuamini baridi hapa ni chini ya 10 degress na huyu jamaa yupo na nguo ya ndani tu na gitaa lake. Watu walikuwa wanamshangaa kwa jinsi anavyoweza kuhimili baridi la hapa. Mimi kwa mtazamo wangu labda huyu jamaa ni kizazi cha Penguin. Mambo ya New York City hayo!

Hili ni gari la zima moto kwa ajili ya emergency katika mji wa North Attleboro kukihitajika msaada wowote kwa wakazi wa kijiji hicho kutokana na baridi. Lakini gari hili limejikuta labda ndo lenyewe litahitaji msaada kutokana na kufunikwa na theluji.

Pata picha kama wewe ndo upo ndani ya nyumba hii na hakuna heat jinsi theluji ilivyoifunika nyumba hii. Hii ilikuwa katika mji mmoja wa Plattsmouth, Nebraska.

Brooklyn Bridge ni Daraja linalounganisha Brooklyn na Manhattan. Watu wakitembea katikati kuelekea Manhattan. Kwa mbali unaweza kuona jengo refu kuliko yote la One World Trade Center likipamba jiji la New York City.
New York City

No comments:
Post a Comment