ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 5, 2014

MSIBA DMV NA TANZANIA


Zainab Buzohera Enzi ya Uhai wake
Dullah na familia ya Buzohera wanasikitika kutangaza kifo cha mpendwa wao Zainab Buzohera kilichotokea jioni ya Jan 4, 2014 saa 2 usiku(8pm ET) katika hospitali ya Lanham, Maryland kama ilivyomila na desturi kupeana pole ndio Utanzania wetu 

Msiba upo nyumbani kwa marehemu  Address ni 5030 57th Ave Apt 303, Blandensburg, MD 20710

Msiba huu ni wote sote

Habari zaidi baadae
 Watanzania wa DMV waliofika hospitali mara baada ya kusikia habari ya msiba ya mpendwa wao wakiwa na sura za majonzi na wengine wakisema ni vigumu kuamini kama picha zinavyoonyesha.
 Watanzania waliofika hospitali mara tu walivyopata taarifa ya msiba wa mpendwa wao wakiwafariji Dullah na mdogo wa marehemu Ngalu Buzohela.
 Abuu wa Swahili Villa Blog akitoa mawasiliano kwa wengine kuwajulisha kuhusu kifo cha mpendwa wao Zainab Buzohera kilichatokea jioni ya Jan 4, 2014 katika hospitali ya Lanham, Maryland.
 Watanzania wa DMV wakiwa na nyuso za majonzi.
Watanzania wa DMV wakimtuliza na kumpa pole mdogo wa marehemu Ngalu Buzohela wa pili toka kushoto wakisaidiana na mume wa marehemu Dullah(kulia).

3 comments:

Ebra said...

Hold tight to memories for comfort, lean on your friends and family for strength, and always remember how much you are loved. R.I.P

Anonymous said...

Inna lillayhi wa inna ilayhi rajuun. Poleni sana, tupo pamoja.
Alu Kalala-Nyang'oro and Julius Nyang'oro

Anonymous said...

Inna lilahi wainna ilayhi rajiun, ya ALLAH mjaalie mja huyu Zaynab mapumziko mema, muondoshee adhabu za kaburini, msogezee malaika wema na umpokee akiwa miongoni ya waja wako wema, ameen. Nawaomba vijimambo waiondoe hii picha ya marehem ambayo yupo kichwa wazi na badala yake waongee na familia kama wanayo picha aliovaa kiislam yaani kujitanda nakadhalika. Kwani mwanamke wa kiialam hatakiwi kuvaa hivi na kuwepo kwa picha hii hapa ni kumzidishia makosa marehem. Tumuombeeni kwa Allah amsameh yeye pamoja nasi kwani hakuna aliekamili. Poleni wana familia na marafiki wote kwa ujumla.
Shukran