ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 4, 2014

SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA TIMU YA VIJIMAMBO


Kwanza: tunapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kuuona mwaka 2014, bila kuwasahau familia zetu kwa ushirikiano wa karibu wanaotupa kila siku kwa kukubali kwao kazi tuifanyayo ya kuhabarishana na wao kuipokea kwa mikono miwili pia tunapenda kutoa shukurani za pekee kwa Kalley Pandukizi, Jojo,  Felix Muzungu, Ebra Nyagali, Cassius, Make Aton, Mwana wa Njenje, Abdul Majid, Walter Minja, Lily Nyalusi, Idd Sandaly, Imma Washiriki wa Kijiwe Cha Ughaibuni, Benja Mwaipaja, Jabir Jongo, Yassin Randy, Ally Bambino, David Ndunguru, Mussa Linga, Dotto Mallongo, Kenyata, Mwinyikheri Mkwavi Make Aton, Hussen Choteka, Ally Mussa, Abdilah Makeo, Kijiwe cha Ughaibuni New York na North Carolina bila kumsahau Sam Malonja wakiwemo wageni waalikwa walioshiriki kwenye kijiwe na Longa na Vijimambo.

 Pili:tunashukuru wadau wa Vijimambo popote pale Duniani kwa ushirikiano mnaotupa saa 24 siku saba kwa wiki kusema ukweli ni faraja iliyoje Mmekuwa wamiliki wazuri wa Blog hii na bila nyinyi Blog ya Vijimambo isingefikia hapa ilipo na tunashukuru sana kwa ukaribu na moyo wa upendo mnaotuonyesha na kufanya kazi yetu ya uendashaji wa blog yenu kuwa rahisi. Tunathamini mchango na mawazo yenu mnayotupatia kila siku ya kuboresha Blog ya Vijimambo ukiona hatujalifanyia kazi ujue muda muafaka haujafika kwani nyie ndio wamiliki wa Blog hii na sisi ni waendeshaji bila nyinyi kazi yetu isingekuwepo, tunashukuru sana na tunaomba mlitambue hilo.


Tatu:tunapenda kutoa shukurani zetu kwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Ujumbe wake kwa kukubali kuhudhuria sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo July 6, 2013 katika ukumbi wa Hampton Conference center

 Nne:tunapenda kutoa shukurani zetu kwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia kwa kukubali mwaliko na hatimae kuhudhuria sherehe ya Uhuru wa Tanzania Bara hapa DMV.

Tano:Vijimambo Blog inapenda kumshukuru aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Maajar kwa kuweza kutambua umuhimu wa mawasiliano na kukubali kuifanyia uzinduzi Blog hii Oct 23, 2010 katika ukumbi wa Mirage pamoja na kwamba haupo tena Marekani lakini unaendelea kuwa karibu sana na Blog hii siku hadi siku tuashukuru sana kwa hilo.

Sita: tunapenda kutoa shukurani zetu kwa Ofisi ya Rais, Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico uliopo Washington, DC, Ubalozi wa Kudumu waTanzania Umoja wa Mataifa New York, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula, Balozi wa kudumu Umoja wa Mataifa Mhe. Tuvako Manongi, Maafisa na wafanyakazi wa Balozi hizi mbili kwa ushirikiano wa karibu mnaotupatia na kuifanya kazi yetu kuwa rahisi.

Saba: tunapenda kutoa shukurani kwa makumpuni mbali mbali Tanzania kwa ushirikiano na ukaribu na Blog hii ya Vijimambo bila kusahau Ethiopia Airline tunasema asante kwa ukaribu wenu.

Nane: Tunapenda kutoa shukurani kwa Masanja Mkandamizaji na Shilole kwa kukubali kujumuika na sisi kwenye mkiaka 3 ya sherehe ya Vijimambo.

Tisa: tunapenda kutoa shukurani zetu kwa Jumuiya za Tanzania za aina zote zikiwemo taasisi mbalimbali za Watanzania nchini Marekani kwa ukaribu na ushirikiano wao wanaoendelea kutupatia yakiwemo makampuni binafsi.

Kumi: tunatoa shukurani kwa makampuni yanayotangaza na blog hii tunashukuru kwa kukubali na kuamini kwamba kutangza kwenye blog hii kutasaidia kukutangaza bidhaa zenu.

Kumi na moja: tunapenda kutoa shukurani kwa Blog zote ndani na nje ya Tanzania kwa ushirikiano wa karibu mnaoutupa Asante na Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awazidishie 7 mara 70.

Mwisho: Tunapenda kuomba radhi kwa yeyote ambaye anafikiria hakutendewa haki na blog hii 2013 aidha kwa kutofurahishwa kwa habari, picha au maoni yaliyowekwa na kusababisha usumbufu wowote. Kwa kuepusha jambo kama hilo lisitokee 2014 tunaomba utujulishe kama kuna habari, picha au maoni yatakusababishia usumbufu tuaomba usisite kutujulisha na sisi waendeshaji wa Blog hii hatutasita kufuta, habari, picha au maoni hayo Asanteni na tunawatakiwa mwaka wenye Amani, Upendo, Mshikamano na Utanzania Zaidi na Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema afungue njia na atusaidie wote tuweze kutimiza malengo tuliojiwekea. Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake, Amina.