Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa
Katika jitihada za kuwapelekea mawasiliano wananchi vijijini na maeneo yasiyo na mvuto kibiashara, serikali imetoa Sh bilioni 17.5 kuyawezesha makampuni ya simu kusambaza huduma hizo.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa, alisema jana kwenye mkutano na wanahabari na kuongeza kuwa fedha hizo ni mikopo kutoka Benki ya Dunia (WB) na nyingine zimetolewa na serikali yenyewe.
Alisema utaratibu huo ulianza kwa kutangazwa zabuni kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kwenye kata 152 zilizopo mikoa 20, wilaya 29 na vijiji 869 vyenye wakazi milioni 1.6.
Alisema baada ya taratibu za zabuni kukamika kampuni nne zilikidhi vigezo na masharti na kufanikiwa kushiriki kupeleka mawasiliano kwenye kata 52.
Kampuni hizo ni Vodacom iliyopeleka huduma kata ya Baray mjini Karatu mkoani Arusha , Tigo ilisambaza kata 19 wakati TTCL ilihudumia 20 na Airtel 12.
Mbarawa alieleza kuwa matarajio ya serikali ni kwamba ifikapo Machi mwaka huu kata zote ziwe zimepelekewa mawasiliano na watoa huduma.
Alizishukuru kampuni hizo kwa kupeleka mawasiliano ya simu kwenye maeneo ya vijijini na yasiyo na mvuto wa kibiashara katika kata 48 kwa gharama zao bila kupewa ruzuku na serikali..
Alisema mbali ya mkopo na WB uliolenga kufanikisha juhudi za kupeleka mawasiliano ya simu vijijini, serikali imechukua hatua ya kutumia fedha zake za ndani zinazotokana na tozo ya asilimia 0.3 kwa pato ghafi la watoa huduma kwa mwaka.
Alibainisha kuwa kampuni za simu ya TTCL, Zantel, Vodacom, Airtel na Tigo zimeshiriki kwenye zabuni hiyo zilizotolewa mwaka jana.
Alisema wizara yake inatarajia ifikapo mwishoni mwa mwaka huu kata 220 ziwe zimepelekewa huduma hiyo na kwamba inaendelea kutafuta njia za kupata fedha na teknolojia rahisi kutoka kwa wadau wa ndani na nje ili taifa liwe na mawasiliano yenye kiwango cha juu ambayo yatachochea uchumi.
Kuhusu usajili wa laini za simu, Waziri Mbarawa alisema zoezi limefanikiwa na kwamba kila mara wanapata taarifa za usajili.
“Natarajia Jumatatu kufanya kikao na watoa huduma wote kwa sababu zipo changamoto zilizojitokeza (bila kuzitaja), hatutaki kurudi nyuma,” alisema.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote, Peter Ulanga, wamekuwa wakitoa ruzuku ya asilimia 30 hadi 70 kwa makampuni ya simu ili yawe na mvuto wa kibiashara.
Aliwaambia wanahabari kuwa kwa upande wao faida ni kukuwa kwa uchumi katika maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment