Kwa ufupi
- Tanzania imekuwa taifa la ajabu na masikitiko yetu ni kwamba mporomoko wa maadili katika jamii yetu umeziba mitima na dhamira za viongozi wetu na jamii nzima kwa jumla kiasi cha kuyaona matendo hayo kama mambo ya kawaida.
Uzoefu wetu wa
muda mrefu umetuonyesha pasipo shaka kwamba mambo mengi yanayotendeka Tanzania hayawezi kutendeka katika nchi nyingine.
Tanzania imekuwa taifa la ajabu na masikitiko yetu ni kwamba mporomoko wa maadili katika jamii yetu umeziba mitima na dhamira za viongozi wetu na jamii nzima kwa jumla kiasi cha kuyaona matendo hayo kama mambo ya kawaida.
Tunayo mifano ya matukio lukuki ya ajabu na ya kushtusha yaliyowahi kutokea hapa nchini lakini yakaonekana kama ya kawaida.
Fikiria wafanyabiashara walioiba mabilioni ya fedha za Epa ambao muda mfupi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2005 walikwenda Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakati wa siku za mapumziko na kukwapua mabilioni hayo kwa njia za udanganyifu. Fikiria wezi hao walivyoahidiwa kwamba iwapo wangezirudisha wasingechukuliwa hatua yoyote.
Ebu fikiria nchi ambayo kiongozi wake anakwenda ughaibuni na kutangaza kuwapo kwa majangili mapapa 40 na kusema kiongozi wao yuko mikoa ya Kaskazini, badala ya kusema hayo akiwa nchini, ikiwa ni pamoja na kuyakamata majangili hayo na kuyachukulia hatua.
Ebu fikiria matukio haya mawili ambapo Waziri Mkuu anatamka bungeni kwamba ni sawa tu kwa Jeshi la Polisi kuwapiga wananchi ‘wakorofi’, huku mkuu wa nchi akikiagiza chama chake cha siasa ambacho yeye ni mwenyekiti kuwapiga wapinzani anaodai wanafanya vurugu dhidi ya wafuasi wa chama chake. Ni nchi gani ambayo viongozi wake wakuu wanaweza kutoa amri hizo za hatari?
Tumesema yote hayo kutokana na kitendo cha ajabu na aibu kilichofanywa na Mwenyekiti wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Dk Emannuel Makaidi cha kufanya ulaghai na kujiwezesha yeye na mkewe kuteuliwa kuingia katika Bunge la Katiba.
Katika utetezi wake, ametoa hoja za kuchefua na kughadhabisha kuwa, kwa vile mke wake naye ni mwanachama wa chama hicho alikuwa na haki ya kuteuliwa kama ilivyo kwa Rais Kikwete na mke wake ambao wote ni wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM.
Tunasema uteuzi huo haukubaliki hata kidogo kutokana na kukiuka taratibu zilizowekwa kisheria kwamba vyama vya siasa lazima viwe na sura ya Muungano katika mfumo na uendeshaji wake.
Ni ujasiri na uthubutu wa kiwango cha juu kujiteua yeye na mkewe kama vile NLD ni mali ya kifamilia. Kudai kwamba aliteua majina ya wanachama wanne na Rais akamchagua yeye na mkewe ni uongo wa kupitiliza.
Hii inaonyesha kwamba zilikuwapo mbinu chafu katika mchakato wa uteuzi huo, vinginevyo wanachama wa Zanzibar wangenyimwa vipi uwakilishi? Hatua ya chama hicho upande wa Zanzibar ya kumtaka Rais Kikwete atengue uteuzi wa Dk Makaidi na mkewe lazima iungwe mkono.
Tatizo hapa ni hatua ya Serikali kuendelea kuvibeba kwa sababu za kisiasa vyama vya siasa vilivyokufa siku nyingi. Ukweli ni kwamba NLD na vyama vingine vingi ambavyo kwa mujibu wa sheria ya vyama ya 1992 vinapaswa kufutiwa usajili wa kudumu bado vinatambuliwa kiasi cha viongozi wake kuingizwa katika Bunge Maalumu la Katiba bila kuwa na sifa stahiki.
Hivyo, wananchi wawe tayari kushuhudia vitimbi vya viongozi wa vyama hivyo ndani ya Bunge. Ndiyo maana tunasema mambo mengi yanayofanyika Tanzania hayawezi kufanyika katika nchi nyingine.

6 comments:
Uajabu wa Tanzania hauishii hapo tu hebu tazama wanavyopinga uraia pacha kwa madai ya huku wataka na huko wataka:( tena wanasema siyo lazima yanayofanyika nchi jirani yafanyike Tanzania; ( ..Tumekuwa wavivu wakufikiria na kuendelea kuwa na ujanja usio na tija ..ndiyo maana tunalia kutengwa na Kenya ,Uganda naRwanda kwa madai ya kutokuwa tayari lakini hatuchukui hatua zozote kubadili mfumo mmbovu wa elimu tulioachiwa na JK Nyerere.. Wenzetu Kenya na Uganda wanatumia kiingereza kuanzia darasa la kwanza ..sisi tumeng'ang'ania mfumo unaoharibu vizazi:( Leo hii msomi wa Tanzania bado amataabika na lugha inayotumika katika soko la ajira (English) WaKenya na Waganda wanatushangaa Sana ..uvivu wa kifikra , ubinafsi ndiyo vinavyotawala Tanzania: ( Tunasheherekea CCM ughaibuni wakati watoto wetu wanakalia mawe madarasani :( watu wamekimbilia posho binge la katiba.. Wabunge wanakuwa na utajiri wa Kutisha kisa ubunge? Mamlaka ziko wapi kuhoji na kutazama vipi watu wanaamka matajiri? MTU Leo anafanya kazi ya ukarani wa bank kesho anateuliwa kuwa mbunge leo anamiliki mgodi wa dhahabu, hotel ndani ya Sinza na bank account za kutisha halafu tunampa heko ! Na vyombo vya usalama vinaangalia? Kweli? Mchawi wa Tanzania ni WaTanzania ..mtandao wa ujangili unaundwa na waTanzania ..:(
Gazeti la Mwananchi Halina ukweli, na tunajua linamilikiwa na mfuasi wa Chadema (irrelevant political party)! Kusema kwamba hakuna nchi nyingine duniani zenye matatizo ya kisiasa ni kuwadanganya Watanzania. Waandishi wa Mwananchi should present facts not fears. Mwananchi newspaper should not be an ideological tool for Chadema with intent to smear and/or harm the welfare of other political groups. Show us statistics that will justify your allegations! I hope your Editors will uphold journalistic standards practised world-wide, instead of disseminating innuendos. I would rather see Dr. Makaidi's NLD political resurgence than poor quality journalism from Mwananchi. Naamini sababu kama hizo ndizo zilisababisha gazeti lenu kufungwa kipindi kifupi kilichopita. A defunct Mwananchi newspaper will be the best thing for journalism in Tanzania.
Mtanzania DC unaonekana hujafika Tanzania siku nyingiume ignore report na facts za report na kushambulia gazeti. Cha uongo hapo ni nini? Yote yaliyosemwa ni ya kweli lakini unashambulia gazeti. Huo ndio unyonge wa fikra unaoendelea kurudisha nchi yetu nyuma kila siku.
Kaka changia point basi znazowahusu wananchi so issue ya chadema na mwananchi apa imetoka wap .hili ndo tatzo la watanzania wengi kwenye vitu vya maana wanaingza politics .
Wewe anon hapo juu nadhani una shida kwenye ufikiri wako au wewe ndiyo Makaidi mwenyewe au member wa familia yake. Unatetea ujinga....eti kila nchi duniani ina matatizo ya kisiasa??? Kwa hiyo ndiyo justification ya kufanya upuuzi. Huu aliofanya Makaidi ni upuuzi ambao nchi nyingine hauwezi kuvumilia, ni kashfa ambayo aliefanya hivyo alipaswa ashtakiwe, ni Kikwete tu anaweza kufanya hivyo ndiyo maana alifanya hivyo. Huwezi kuwafanya watanzania wote wajinga, kwa akili yako wewe anon unaona hiyo ni sawa? Kama jibu ni ndiyo, nakwambia una shida kubwa!! Nyerere, Mkapa, Mwinyi wasingeweza kufanya huo upuuzi, huyo Kikwete wako tu. Umeambiwa unatakiwa uwakilishi wa sehemu zote za muungano, wewe Makaidi unapeleka jina la mkeo....hivi credibility yako ipo wapi? Hilo jina la mkeo lisingetakiwa hata lipendekezwe! Ungekuwa mtu wa maana iwapo usingependekeza la kwako kwani kuna vijana wengi walio na uwezo kwenye chama kuliko wewe. Usilaumu gazeti la mwananchi, limefanya kazi yake kwa kufichua ukweli.
Mdau umechemsha..unataka kutuambia kuwa matatizo ya kisiasa nchi nyingine yawe tiketi ya kusamehe matatizo yetu? Kwa taarifa yako Gazeti la Mwananchi ndiyo lililofichua Richmond, wizi wa kutisha EPA na uchafu mwingi tu unaotokea kila uchao ndani ya serikali ya CCM
..tatizo lako wewe hupendi kuona CCM ikikosolewa :( Demokrasia ya kweli haichukii kukosoana..CCM ndiyo chama tawala kwa hiyo kama hutaki tukikosowe turudishe kwenye chama kimoja na fikra za kinafki za zidumu fikra za JK Nyerere... Kaa pembeni na kwa taarifa yako hii ni vijimambo acha ulimbukeni wa kutuchanganyia lugha..
Post a Comment