Huyu alikua muanzilishi haswaa wa Afro-beat.Alikua
Star wa kimataifa kutoka Nigeria aliyeenda chuo huko Los Angeles ,
Marekani kusomea udaktari akajikuta anaingia kwenye muziki. Kuti
alifariki tarehe 3 ,August 1997 huku akiwa ni mwanaharaki mkubwa wa
ukimwi na waziri wa afya wa zamani.Watu zaidi ya millioni moja
walihudhuria msiba wake.

Rock Hudson
Rock alikua ni mchekeshaji wa miaka ya zamani na kifo chake cha Oct.
2, 1986 ndio kilishtua wengi kuhusu Ukimwi.Hapa ndipo rafiki yake na
star mwenzake Elizabeth Taylor alipoamua kutumia maisha yake yote
yaliyobaki kufanya research kuhusu ukimwi.

Freddie Mercury
Alikua mmoja kati ya waimbaji wa bendi maarufu kabisa duniani miaka
ya 80 hadi 90, Queen. Mercury alikufa akiwa na miaka 45 ilikua november
24 mwaka 1991. Siku chache kabla hajafa Mercury aliamua kujitangaza
kwamba ni muathirika wa ukimwi.

Arthur Ashe
Huyu alikua ni mcheza tennis maarufu sana duniani. Alipata ukimwi sio
kwa njia ya kujamiiana kama unavyofikiria bali ni kwa kuchangia damu.
Arthur alikufa akiwa na miaka 49, February 6 mwaka 1993.

Eric “Eazy-E” Wright
Alikua kwenye kundi la Rap lililoitwa N.W.A. ambapo alikua pamoja
na Ice Cube and Dr. Dre.Waliuza mamilioni ya albums marekani hadi hapo
March 26 mwaka 1995 Eazy-E alipofariki kwa Ukimwi.

Kwa Bongo uwazi wa gonjwa hili bado haujawa mkubwa na kuna baadhi ya
watu maarufu wameondoka kwa gonjwa hili lakini hakuna taarifa
zozote.
BAKI NJIA KUU OGOPA MICHEPUKO !!!
No comments:
Post a Comment