ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 8, 2014

WAKUTWA WAKIKOJOA KWENYE MASINKI YA KUNAWIA MIKONO UWANJA WA TAIFA.

Dar es Salaam National Stadium , urinating in the hand/face washing sinks. Huu ni ushamba na ulimbukeni, these thugs need induction before getting into the stadium.

Jamani kwa wale mnao simamia uwanja huu bora muweke toilet attendants maana hii ni aibu

DJ SEK BLOG

8 comments:

Anonymous said...

Mimi nilikuwepo kwenye mstari huo mrefu tu watu wanasubiri zamu ya kukojoa, there were no toilets, either you use the sink or pee on the floor. Na nyninyi mnaoishi ughaibuni mnafikiri nynyi tu ndio mnajua ustaarabu. You got to do what u need to do in this situation. We je hujajisaidia kweneye vishaka kabla hujaenda ulaya? Come on Man!!!

Anonymous said...

hata tufanye hatutabadilika. Exposure ni muhimu sana

Anonymous said...

Huu uwanja umejengwa na walipa kodi kwahiyo ni uwanja wetu wote. Inakuwaje watu wanafanya vituko kama hivi kwenye mali yetu tunawaachia?

Anonymous said...

Kama wanang'oa viti uwanjani timu zao zikifungwa sembuse hayo wayafanyayo? Ushamba si ushamba bali wakati mwingine ni kukosa elimu na utu wa kibinadamu. Hawa ni wanyama, their thinking capacity is below 34% because more than 50% of IQ's test grades states how selfcontrols they coul have in their lives. Wadau changieni hili.

Anonymous said...

Namba moja unaonyesha wazi kama wewe ndio ulikuwa hapo mahali, this is nonsense!! Kwa akili ya mtu kichwani na macho mawili kweli unaweza kufanya jambo kama hili na ukijua kuna gharama iliyotumika kuweka kile kifaa!!! kama nyumbani kwako unaweza kufanya hivi??? jiulizeni na mjijibu wenyewe!! kwani maeneo ya kuzunguka uwanja hakuna vyoo kwenye mabaaa.. Tuacheni ulimbukeni. asante.

Anonymous said...

Kweli akili ni nywele kila mtu ana zake.

Anonymous said...

Binadamu tumepewa akili ya kufikiri tofauti na wanyama. Kama kuna binadamu anaona ni sawa kukojoa kwenye sink la kunawa mikopo basi ana tatizo kubwa la uwezo wa kufikiri, haijalishi nchi anayoishi. Hao wanaosema kulikuwa na misururu mirefu mbona hawakojoi kwenye daladala zinazochukua hadi masaa matatu hadi posta mpya na huko ndani ya daladala hakuna vyoo, kama watu wanavumilia kwa masaa wanashindwaje kuvumilia kwa dakika 10? Tuwe wastaarabu na wakweli....nashangaa watu wengine waliotoa maoni wanawasema watanzania wanaoishi nje bila sababu....wamehusika vipi hapo? Huo ni kukosa ustaarabu wa kuwashambulia hao watanzania wasio na kosa, kwani aliyepiga picha alisema anaishi nje? Au hao wanatuaminisha kuwa watanzania wote walio ndani wana ustaarabu wa kukojolea masinki ya kunawa mikono? Kama kuna mtu yoyote yule anatetea kukojoa au anayekojoa kwenye masinki basi uwezo wake wa kufikiri una matatizo inaonekana hao binadamu wanatetea na wavunjaji wa viti vya uwanja vilivyojengwa kwa mabilioni tena kwa mikopo.

Anonymous said...

Katika jamii yetu ya kitanzania swala la choo na usafi kwa ujumla huwa liko chini ya orodha ya vitu vya muhimu. kwa kweli nakubaliana na kila mmoja wenu kwa namna tofauti. Kwanza, utakuwaje na mkusanyiko wa watu zaidi ya elfu hamsini bila kuwa na idadi tosha ya vyoo, unataka wakajisaidie wapi ? kwenye kopo au... Pili kama kuna vyoo vya kutosha na hawa majuha(jamaa) wakaamua tu kwa utashi wao kukojolea masinki ya kunawia mikono basi hawana tofauti yoyote na wang'oa viti au wale majuha wanaotumia kinyesi kuandika majina yao kwenye kuta za vyoo. Ila la msingi ni kwa sisi wabongo wenyewe, kama sehemu haina huduma muhimu kama choo kwa nini tunaenda ? Najua wenzangu na mimi watasema ooh!!! mpira. Mbona mererani kuna uwezekano mkubwa tu wa kuitoa na si kila mtu anaenda kila kukicha tunalia hali ngumu. Kama unauwezo wa kujua hatari iliyopo ukaacha kwenda kutafuta pesa, mpira vile vile unaweza ukauchinjia kwani nini bwana...
Wenu katika ujenzi wa taifa, Very Very Dirty Southerner.