- Nimeombwa mara nyingi sana kuigusa hii topic lakini nilikuwa sijawahi kwa sababu sijawahi kuwa convinced kwamba waombaji wapo serious, lakini leo nimeamua kuigusa kwa sababu naamini ni the right time nikajaribu japo kuwasaidia mawazo kidogo ndugu zangu wabongo huko nje ambako na mimi nilikuwa mkazi wa muda mrefu sana.
- Guys mlioko nje tatizo kubwa linalowasumbua na hii ishu ni kukosa kwenu hoja za msingi za kuwashawishi wananchi huku Tanzania kuhusu hiyo ishu, halafu pili kukosekana kwa umoja wenu on this ishu pia inachangia sana katika kuwachelewesha kupatikana kwa solution ya the ishu. Mpaka leo mmeshindwa kuelewa kwamba Tanzania sasa inaongozwa na siasa za uchumi, sijaona popote mkijenga hoja ya Taifa letu litafaidika vipi kiuchumi iwapo mtapatiwa hiyo dual citizenship? Wekeni mahesabu tuone wabongo wote huko nje kwa ujumla wenu kipato chenu kwa mwezi ni hela ngapi, kwa mwaka ni hela ngapi, halafu onyesheni kwa mifano hai kati ya hizo mnatuma ngapi bongo na zinalipa kodi za bongo kiasi gani, halafu wekeni mifano ya nchi zingine kwa mahesabu hayo hayo kama ya kwenu.
- Tatizo lingine mlilonalo ni hamna umoja on this ishu, wengi wenu mnaonekana mnajaribu tu kuitumia hii ishu na platform yake kutafuta umaarufu na vyeo vya siasa hapa bongo, mara ya mwisho niliwahi kukutana na dada mmoja akaniambia yeye ndiye mtu wa Diaspora katika ofisi ya Waziri Mkuu so I was like how come simfahamu wala sijawahi kumsikia, amewahi kufanya au kusema nini serious mpaka Taifa likatikisika kuhusiana na ishuz za Diaspora? Wengi wenu mkija hapa bongo mnajulikana sana kwamba shida yenu ni kutafuta vyeo tu na kupiga picha na viongozi wa juu wa Taifa basi, badilikeni ndugu zangu kama kweli mko serious mnataka hii ishu ikubaliwe.
- Kwanza jiungeni wote muwe na one say, halafu jifunzeni mbinu za lobbying ni lazima mtumie watu huku bongo ambao wana nguvu za ushawishi kwa viongozi wahusika na maamuzi, halafu acheni tabia yenu kujifanya kujua sana human rights, nimeona mijadala yenu mingi sana hamko humble enough as watu wenye shida, naona wengi mnajifanya kujua sana hizo attitude zenu za Ulaya huku ni bongo watu wana mambo mengi sana ya maisha yao they could carelesss na hiyo ishu yenu, sasa mnapokuja na bullying tatctis za kujifanya kujua sana kama tabia za Ulaya huku mnaonekana wajinga flani hivi au vikatuni hivi, badilikeni kaeni chini on a serious note watumeni watu wenye adabu na uvumulivu na waelewa tafuteni hoja nzito zenye namba za kichumi, halafu wacheni tamaa za kijinga za jinga za kukimbilia kupiga picha na viongozi tu, tafuteni watu wanaoweza kuwasaidia huku bongo, ama sivyo mtaendelea kupigana na vivuli vyenu wenyewe huku bongo maisha sio mchezo watu wapo busy sasa kwa nini wapoteze muda na ishu ambayo haonekani kuwa na mashiko yoyote na maisha yao ya kila siku, so badilikeni people!!
Le Mutuz big Show
18 comments:
Acha porojo na chuki binafsi kupiga picha na viongozi na hili swala hakuna uhusiano.
Nafikiri mabadiliko yanahitajika kwako kabla hujatuambia tubadilike :( Hivi kunaulazima gani wa kuchanganya lugha wakati unafahamu vizuri lugha ya mama yako? Halafu lugha ya watu ndiyo umeiboronga Kwelikweli:(
Kwan taarifa yako na wengine wasiofahamu nguvu za hoja ya uraia pacha Raisi Kwikwete anafahamu vizuri kilio chetu na yupo nyuma yetu ..Mwingine ni pamoja na Waziri Membe ..ndiyo maana tunamwakilishi kwenye bunge la katiba ..Rais anafahamu mchango wetu ndiyo maana anatujali na ni kiongozi anaeipenda nchi yake na raia wake...ukituona kwenye picha na Rais/mawaziri endelea ukurasa wa pili usikonde kwa picha.
usituchanganyishie lugha, tumia kiswahili au kingereze.Mnanakera sana kuchanganyisha lugha namna hii, yaniii.
huyu mtu anaonekan an hasira na na watu. alikuwa deported nini?....kwani alianza topic yake vizuri ghafla akavuruga kwa kuanza kuwapiga watu madongo. hili swala la dual citizenship sio tu la watu anaowajua yeye.kama ana hasira na watu bora atumie njia nyingine ya kuwaponda
Wewe mleta mada,acha kupayukapayuka. Sijui hata shule umesoma wapi? Andika insha ya Kiswahili au Kiingereza kilichonyooka,usituchafulie hali ya hewa!Unaonekana kuwa na hasira au chuki na wana-diaspora, huna hoja za msingi.Tuondolee ushuzi.
Mwandishi-Le mutuz big show-tafadhali andika jina lako halafu maswali uliyauza ujabiwa with scienfic evidence na sio kwa kubuni. Sisi hatuombi kazi Tanzania, tunataka kuwaelimisha watanzania- knowledge transfer, tunataka kuwapa kazi watanzania, tunataka watanzania wawe na afya bora,watanzania waishi maisha bora kama watu wengine duniani. Tunataka kuwaelimisha watanzania jinsi kuhifadhi mali ya asili kwa faida ya nchi na vizazi vijazo:Elimu na experience tuliyoipata huku huwezi kuifananisha pesa. Kama wewe ulikaa huku ugaibuni kwa miaka mingi, hukenda shule, hukupata experience yeyote, hukuwa mwachanma wa jumuiya ya watanzania, hukuchangia mchango wowote kwenye jumuia yako, basi usijifananshe wewe na wegine ambao wana upeo zaidi. Ukisha andika jina lako, utapewa statistics zote-kama utaweza kuzisoma- ambazo zitaoyensha hili swali la uraia pacha litapitishwa kwenye Katiba Mpya bila matatizo.
United we Stand.
Temba
Mbona hayo madai ya kichumi unayoyazungumza Kadari Singo ameyaweka wazi na ameyachambua kitaalamu kabisa. Sidhani kama madai yako ya kupiga picha na viongozi wa juu ina msingi wowote kuzuia dual citizenship. Wewe ndiyo inabidi ubadilike. Diaspora kuna watanzania zaidi ya milioni mbili. Kwahiyo unayo mifano milioni mbili ya wanadiaspora kupiga picha na viongozi wa juu. Let us say for the sake of the argument, you are right. Kuna uhusiano gani kati ya wanadiaspora milioni mbili kupiga picha na viongozi wa juu na suala Zima la dual citizenship. Inasikitisha sana kuona elimu uliyopata pamoja na exposure inakufanya uzidi kuwa mpumbavu.
Ndugu mwandishi, nakala yako nadhani imepoteza nguvu ya ushawishi pale ulipoamua kutumia kiingereza na Kiswahili kwa wakati mmoja. Lugha hizi mbili zinafanya hoja zako zionekane nyepesi na zisizostahili kutiliwa maanani. Vile vile, pale unaponukuu watu kwa mfano "nimekuwa nikiombwa sana niandike kuhusu mada hii" ingependeza kama ungetaja kundi la watu waliokuomba vingenevyo hii nakala inaonekana kama maongezi ya watoto wa secondari. Pamoja na mengineyo, mada nyingi ulizozipitia katika nakala hii ni za kawaida sana na suala la watu kuungana na kushinikiza serikali si jambo geni kwa mtu yoyote. Kwa ujumla nakala yako haisimamishi kope za mtu yoyote kutokana na wepesi wake.
Wana-Diaspora wenzangu, inabidi tutulize vichwa vyetu. Wengi hapo juu mmetoa maoni yenu, na wengine mmemtukana, kumkosoa na kumweka chini (despised) huyu mwandishi kama hana akili...Hilo siyo suluhisho. Kwa bahati mbaya wengi hatumjui, lakini baada ya kutafakari aliyoyaandika, naona kuna machache yana msingi. Huku Ughaibuni kuna kambi mbili za Wana-diaspora. Kati ya milioni mbili (kama inavyodaiwa), miongoni mwetu tupo wengi ambao hatuoni umuhimu wa "dual citizenship". Wengi tumesoma kama bwana Dr.Temba nakadhalika na hatuhitaji "scientific evidence" kwenye suala hili. Ukweli wa wazi ni huu: Kama sisi wana-diaspora TULIUKANA URAIA wa TANZANIA, na kuomba uraia wa nje (USA, UK, Sweden, etc.) kwa sababu ambazo kila mmoja wetu anazo binafsi, Kwa nini sasa tunavurugika kimawazo na kuanza kujilaumu? Tanzania haijatukana hata, bali sisi ndiyo tuliamua kuikataa. Tanzania inamkaribisha yeyote ambaye yupo tayari kuirudia, hivyo basi dawa ya hili suala ambalo tunaliwekea ugumu ni rahisi sana: Tuukanushe URAIA WA NJE ambao tumeupata na turudi salama Tanzania. Kama Umeelimika kama mimi, basi Elimu na ujuzi wetu utalisaidia sana Taifa letu. Kama umejitengenezea rasilimali, basi Taifa litafaidika pia. Mdau mmoja amesema vyema, kuwa anataka "knowledge Transfer". Nadhani utafanya vyema sana na utaalamu huo ukirudi Tanzania. Fani yeyote itasaidia nchi..Wahandisi, Madaktari, Wahasibu, Maprofesa, Watafiti, Wauguzi, n,k. sote tunahitajika na tunakaribishwa kwetu tulikotoka bila chuki wala porojo.
WILLIAM, Nadhani sasa ni wakati wako kutulia Dar na uwe mkia wa watu wengine kwani Marekani imekushinda na umekimbia familia yako. Acha watu wakulishie familia na hao hao ndio unaotukana, tafadhali tulia.Endelea unapiga picha na wake na mabibi za watu sasa hivi unaitwa William ntakuoa. kwani kila umuonae unamwambia nitakuoa.Achana kabisa na Diaspora. Msichana alioko ofisi ya Waziri mkuu unamwandama nini? Ni naaamini ni mjuzi kuliko wewe na anayo nafasi nzuri kuliko wewe ambae unashinda Falcon Restaurant hapo Lumumba kutafuta madili ili upate Cha kula. Lakini cha kutuma kwa familia hunaaaaa.Tunawalisha sisi wana Diaspora. Diaspora oyeeee!!!
mimi naomba nikueleze ukweli ndugu wewe unaejiita mtoto Malechela lakini usiyepata malezi ya Malechela..Kwanza naomba niwajulishe wadau historia yako labda wengi hawakujui.Wewe ulikua ukiishi Marekani kwa paper za mke wako,pamoja na mke wako kukusaidia kupata vibali vya kuishi Marekani ukamtenda na akajitoa kwenye kesi yako ikabidi upewe diportation(kufukuzwa)..kwa maana hiyo ulifukuzwa marekani kwa maana nyingine bado ulikuwa unaitaka marekani...nimeweka kisa hiki samahani ili wadau waelewe kwamba wewe unahasira lau kama sio kuachana na mke wako au ungelikuwa na karatasi mpaka leo ungekuwa marekani na ungekuwa upande wetu kuomba uraia wa nchi mbili...cha kwanza nilichogundua una JEALOUS baada ya kuyaharibu yako....na umeshia kumtukana x wife wako kwenye mablog umesahau wema wote aliokufanyia na hata kufikiria unawadhalilishia mama yao watoto wako...umetelekeza watoto wako halafu unasimama mbele za watu kusema hata aibu haoni..mwalim nyerere alisema kiongozi mzuri huanzia kwenye familia yake...na ndio maana nikasema kwaninavyomjua mzee malechela ninahakika wewe sie mwanawe au hujapata malezi yake..amakweli ukubwa wa kichwa sio wingi wa akili..una bichwa kubwa na kipara lakini bure kaka
Huyo mwandishi mpumbavu ni somebody Le mutuz sijui kitu kama hicho, ni kubwa jinga moja hivi alikimbia huku US na anasakwa kwa child-support vile vile, msiumize vichwa kwa hili jinga guys please!! Mkilijibu mtaonekana wote wajinga. Pumbavu fulani hivi.
Anonymous 10:16, umetoa maelezo ya kutosheleza kabisa kuhusu huyu jamaa. Nataka kuongezea kwamba akili zake siyo nzuri, na zimeharibika zaidi aliporudi TZ. Watu wameshajua kwamba ni mental retarded, kwa hiyo wanamchukulia accordingly. Anajaribu kujifanya anajua kila kitu wakati hana analofahamu. Watoto wa Mzee Malecela wakiume waliotangulia mbele ya haki, Mungu awaweke mahala pema peponi, hawakuwa kama huyu jamaa. Waliobaki ni wasomi, wanahangaika na maisha yao, wala huwezi kusikia wanapayuka hovyo kama huyu jamaa.
Walengwa huyu Le mutuz amesema vizuri mwazoni japokuwa ametoka nje kidogo mwishoni. Nadhani ameelezwa vya kutosha. Kuna mambo aliyozungumzia hapo mwanzoni na mimi kama mdau naamuunga mkono.
1. Suala la umoja wa diaspora ughaibuni bado lina kigugumizi tumeanza na kuandikisha "pettition ya dual" namba bado iko chini tumekuja na suala la michango kutumia tovuti ya "gofundme" bado to kwenye hela chache. Sasa hapa lazima tujiulize kuna tatizo gani.
2. Suala kujenga hoja zaidi nadhani mwakilishi wetu Kadri amezielezea hizo basi tuendelee kuziboresha zaidi na kuweza kuwafikia kila mmoja wetu. Nahamini kila mmoja wetu akilivalia njuga hili swala tutafika pazuri. Uhamasishaji bado mdogo sana ndio maana wengi wa diaspora ukiwa uliza wana majibu madogo kuhusu urai pacha. Hawezi kutetea hoja. Tutumia jumuia zetu kwenye kufanya hizi kampeni na makongamano.
3. Nadhani kwenye sherehe zinazofanyika kama hii ya muungano tuwe na dawati na watu watakao zungumzia suala hili. Nadhani sikuku ya TANO Ladies ilikuwa ni mojawapo ya kuanza hizi campain zetu.
Wadau tuendelea kupiga debe suala ni la wote hili.
Le Mutuz anawakilisha wenye hasira waliokosa mbivu! sis hapa tunataka haki zetu, hatuhitaji kuonewa huruma maana watu wengi walioko nje kichwani wako safi. Kweli tunaishi vizuri na watoto wetu wanasoma kama watoto wa Rais au mawaziri na wabunge bongo. Je hiyo ni dhambi ya kutuhukumu? sis hatujawahi kuua tembo, hatujawahi kurichmond, hatujawahi ku EPA, hatuchakachui wabongo wenzetu, hatuuzi unga kinondon...Ombi langu sheria hiyo iende mbali kwa kuongeza watoto wa viongozi na wabunge wasome pale pale bongo ili kuonyesha kweli wanachukizwa na watu kukaa nje ya nchi
.
nilisoma kwanza hizi comment zenu zote nikasema jamani sijui huyu wanaye mlaumu ndo nani wanaye muita le mutuz big show nikasema saa nisome mada aliyoandika.
kwa kweli nampongeza sana alivyoandika hata kama le mutuz big show atakuwa amefukuzwa marekani kwa child support anatafutwa na mengi mengi tu mliomtukana namunga mkonoa
je mnataka hii dual citizen kwa faida ya nani? watanzania waliopo huku nyumbani ambao ni walalahoi mtawasaidiaje?
je mnalisaidiaje taifa letu huku nyumbani?
na kwa nini walalahoi huku nyumbani wakupigiyeni debe kwa hii isuue
nimekubaliyana naye 100 percent na le mutuz big show msimtukane bure jibuni hayo maswali si eti mnaleta longa longa zenu scientific proven, sijui hatuuzi unga kinondoni sijui hatu ja richmond etc jibuni maswali hayo
ukiangalia sana mnataka dual citizen kwa ajili ya manufa yenu mle keki marekani na huku bongo mje mlee keki pia kwa mikono miwili kwa uroho wenu
kwa taarifa yenu mimi si mtetei lakini nimeona bora mjibu maswali hayo kama mnamuda.
na tena mimi niko msafi nina uraia wa marekani na wala sina taabu ya kutafuta tena wa kibongo.
mungu mkubwa namshukur kwa hili na wala sina kashfa yeyote na mke wangu na watoto wangu tunaishi salaam tu
aliye toa historia ya le mutuza namkubali sana tena namshukur sana kwa kutoa issue yake
hata na mimi nilikuwa sijui le mutuz big show alikuwa akiishi kwa papers za mkewe na kupata kibali kweli hana shukurani huyu bora amefukuzwa marekani akakaen huko kinondoni na kufagilia demu katika ofisi ya waziri mkuu na akika akijua hatompata si mjinga yeye kama unavyofikiria
Post a Comment