.jpg)
Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic 'Loga'
Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic 'Loga', amesema kuwa timu yake haitakuwa ngazi ya Azam FC kuukalibia ubingwa msimu huu na wamejipanga kuwashangaza kwenye mchezo wao wa kesho utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa.
Loga, alisema kuwa pamoja na kuwa kikosi chake kina kazi kubwa mbele ya Azam FC, bado anaamini wanaweza wakapata ushindi kwenye mchezo huo muhimu zaidi kwa Azam FC katika mbio zake kuelekea kwenye ubingwa msimu huu.
Kocha huyo alisema kuwa kwake aangalii timu yake inashika nafasi ya ngapi kwenye msimamo wa ligi kuu badala yake anaziangalia zaidi pointi tatu muhimu.
"Nataka tushinde, sitaki kuangalia tunashika nafasi ya ngapi au tunacheza na nani, Azam ni timu nzuri na ipo kwenye mbio za ubingwa na watakuja kwa lengo la kushinda, tumejipanga kuwashangaza uwanjani," alisema Loga.
Aidha, alisema kuwa mchezo wa kesho wao wanauchukulia kwa uzito sawa na michezo mingine na hivyo wamefanya maandalizi kuhakikisha wanapata ushindi.
Loga alisema kuwa amefanya marekebisho ambayo aliyaona kwenye mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union walipolala kwa goli 1-0 kwenye uwanja wa Taifa.
"Moja ya tatizo letu ni kushindwa kutumia nafasi tunazozitengeneza, nimefanyia kazi suala hilo na nategemea mabadiliko kwenye mchezo wa Jumampili (kesho)," aliongezea kusema loga.
Loga, alisema kuwa hofu yake ipo kwa baadhi ya wachezaji wake ambao hawapo kwenye hali nzuri kiafya kutokana na kuwa majeruhi.
Wachezaji ambao uwenda wakaukosa mchezo wa kesho ni pamoja na mfungaji bora wa timu hiyo, Amis Tambwe pamoja na beki wa kati, Joseph Owino.
Hata hivyo, Loga, alisema kuwa anaamini wachezaji wengine watakaopewa majukumu ya wachezaji hao majeruhi wanaweza wakaifanya kazi kikamilifu.
Kuelekea kwenye mchezo huo wa kesho Loga, alisema kuwa anaiheshimu Azam kutokana na soka wanalocheza na watacheza kwa tahadhari kubwa kwenye mchezo huo.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment