kutoka kushoto Dkt. Grace Mallya kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi. Grace Mwangwa Mtaalamu wa masuala ya Jinsia, Wizara ya Fedha na aliyekaa nyuma ni Bi. Constacia Gabusa Kaimu Mkurugenzi -(Jinsia) Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, wakifuatilia hotuba ya Waziri.
Mhe. Sophia Simba ( Mb) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, akielezea uzoefu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs) ni katika Mkutano wa 58 wa Kamisheni kuhusu Hali ya Wanawake unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Waliokaa pamoja na Mhe. Waziri ni Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi. Bibi. Anna Maembe, Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Bibi. Asha Ali Abdulla, Katibu Mkuu, Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Ujumbe wa Tanzania unavyoonekana katika ujumla wao, wa kwanza ni Katibu wa Waziri, Bi Teodosia Mbunda akijadiliana jambo na Mhe. Jaji Iman Aboud
Bibi. Mwanaidi Saleh Abdulla, Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Fatma Mbarak Hashim Mtaalam masualaya Jinsia,( Zanzibar), Bw. Seif Shaaban Mwinyi, Kamishna na mratibu wa shughuli za Idadi ya Watu, Tume ya Mipango- (Zanzibar) na aliyekaa nyuma ni Bw. Adam Hans Kadege, Mtakwimu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Tanzania imewakilishwa vizuri katika mkutano huu kwa kuwa na wajumbe kutoka pande zote za Muungano.
Wajumbe wengine wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri. Kutoka kushoto, ni Bi. Joyce Mlowe kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi Mhaza Gharibu Juma, Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti, Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto - Zanzibar na Bi. Halima Abdulrahman Omar, Mtaalamu wa Jinsia, Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto- Zanzibar . pamoja na kuhudhuria majadiliano ya mada kuu kuhusu mafanikio na changamoto za utekelezaji wa MGDs, wajumbe wa Tanzania pia wamekuwa wakishiriki kikamilifu katika majadiliano ya mada nyingine nyingi zinazofanyika katika mikutano ya pembezoni ( side-events)
Na
Mwandishi Maalum
Wakati
Mkutano wa 58 wa Kamisheni kuhusu Hali
ya wanawake, ukiwa umeingia wiki yake ya pili,
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
imeeleza kwamba imejitahidi na imefanikiwa kufikia
baadhi ya Malengo ya Maendeleo
ya Millenia hata kabla ya mwaka 2015.
Waziri
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,
Mhe. Sophia Simba ( Mb) ameyasema hayo siku ya jumatatu wakati Tanzania ilipopata fursa ya
kuielezea jumuiya ya kimataifa uzoefu wake katika utekelezaji wa MDGs na changamoto ambazo bado inaendelea kukabilina nazo katika
baadhi ya malengo.
Mhe.
Sophia Simba, amesema Tanzania imefanya vizuri katika malengo nane kati ya nane ingawa bado inakabiliwa na changamoto
katika baadhi ya maeneo ambayo alielezea pia namna serikali inavyojipanga
kukabiliana nayo.
Kwa
wiki mbili sasa, wawakilishi wa kutoka
nchi mbalimbali duniani zinazohudhuria
mkutano huu hapa Umoja wa Mataifa,
wamekuwa wakipashana habari na
wakubadilishana uzoefu kuhusu masuala yahusuyo haki za wanawake, za mtoto wa kike
na ustawi wao na maendeleo yao.
Aidha
wawakilishi hao wamekuwa
pia wakiijadili mada kuu ya
mkutano huu ambayo ni mafanikio na changamoto za utekelezaji wa Malengo ya
Maendeleo ya Millennia, ambapo kile nchi imekuwa ikitoka uzoefu wake.
Baadhi
ya malengo aliyoeleza kwamba Tanzania
imefanya vizuri ni pamoja na lengo
namba mbili linalohusu fursa ya elimu ya msingi kwa watoto wote na kwa kuzingatia uwioano wa
kijinsia.
Aidha
akabainisha pia kwamba Tanzania imefanya vizuri katika lengo
la tatu kuhusu fursa sawa za
kijinsia na uwezeshwaji wa wanawake ambapo alitolea mfano ongezeko la
wanawake katika vyombo vya utoaji
maamuzi kama vile Bunge na Baraza
la Wawakilishi. Na katika
sekta ya elimu ya sekondari ingawa
uwiano huo unapungua kuelekea
elimu ya juu
Waziri
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
akielezea zaidi mafanikio ya utekelezaji
wa MDGs, ameeleza pia kwamba kumekuwa na mafanikio ya kuridhisha katika upunguzaji
wa vifo vya watoto wachanga chini ya
miaka mitano kwa pande zote mbili za
Muungano.
Hata
hivyo licha ya mafanikio ya kuridhisha
katika eneo hilo, Waziri Simba anasema
bado watoto wanaendelea kupoteza maisha kwa maradhi yanazulikia kama
vile malaria na kuharisha.
Kuhusu lengo namba tano kuhusu
upunguzaji wa vifo vya wanawake wajawazito, Waziri anasema, eneo hilo bado linachangamoto
nyingi na kwamba kasi yake ni ndogo.
Ametaja
baadhi ya changamoto zinazolikabili eneo hili kuwa ni uhaba wa
wataalamu, eneo ambalo anasema tayari serikali inalitafutia
ufumbuzi, ukosekanaji wa huduma za
upasuaji wa dharura eneo ambalo amesema serikali pia inalifanyia kazi kwa
kujaribu kuviwezesha vituo vya afya kuwavipatia vifaa na wataalam
Kuhusu lengo la sita linalohusu huduma za afya, Tanzania, kwa mujibu wa Mhe, Waziri, bado inachangamoto nyingi katika
kukabiliana na maambukizi ya virusi vinavyosambabisha ugonjwa wa ukimwi,
malaria na Kifua kikuu magonjwa ambayo yanagusa sehemu kubwa ya jamii.
Akasema
serikali imejitahadi sana katika kuyadhibiti magonjwa haya , kiasi kwamba kumekuwapo na udhibiti wa maambukizo miongoni mwa watu wazima.
Kuhusu
lengo namba saba linalohusiana na Mazingigira endelevu, pamoja na
huduma za maji safi na salama, Waziri
anasema, bado kuna tatizo kubwa la upatikanaji wa maji safi na salama hasa
maeneo ya vijijini.
Mhe.
Waziri Simba anabainisha kwamba
changamoto kubwa kwa Tanzania iko
katika utekelezaji wa lengo namba moja, linalohusu utokomezaji wa umaskini uliokidhiri na njaa.
Pamoja
na kuelezea mafanikio na changamoto za utekelezaji wa MDGs,
Waziri Simba, amesema
Tanzania inaunga mkono msimamo wapamoja wa Umoja wa Afrika, unaosisitiza kwamba usawa wa jinsia na uwezeshwaji wa
wanawake, uwe lengo linalojitegemea katika
Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu baada ya 2015 ( SDGs).
No comments:
Post a Comment