Wananchi wa Tanzania wamepongezwa kwa kufikia miaka 50 ya Muungano huku wakiulinda na kuuimarisha mpaka Leo.
Hayo
yamesemwa na Balozi Job Lusinde ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya
kutayarisha katiba ya Muungano Hivi karibuni Mjini Dodoma.
Balozi Lusinde ambaye pia
alikuwa Waziri wa serikali za Mitaa katika Baraza la kwanza la
Tanganyika mwaka 1961, baada ya kupata Uhuru amesema kwamba madhumuni
ya kuanzisha Muungano huo ilikuwa ni kuonyesha mfano ili siku moja
uwepo Umoja wa nchi za Afrika.
“Wakati tunaugana na Zanzibar
kulikuwepo upepo wa kuwa na Shirikisho la Afika Mashariki, hivyo ilikuwa
rahisi kuanza na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Kama mfano mkubwa
wa kimatendo ” alisema Balozi Lusinde.
Aliendelea kusema kwamba
madhumuni mengine yalikuwa ni kuuimarisha uchumi wa nchi hizi mbili
kwani kabla ya Muungano Zanzibar ilikuwa na watu 300 na Tanganyika
ilikuwa na watu 8,000,000, hivyo baada ya kufunga na uchumi ukiwa
unategemeana na wakaunganisha nguvu kiuchumi , jambo ambalo lilikuwa
faida kwa nchi hiyo mbili.
Aidha, Balozi Lusinde alisema kwamba wakati wa kuungana walifikiria suala la usalama wa nchi hizi mbili, kwamba ni muhimu hivyo kwa kuungana kutaweza kuimarisha usalama. Suala la mwingiliano wa kijamii pia lilichochea kuungana kwa nchi hizi mbili. “kulikuwa na mwingiliano mkubwa awa kijamii kama vile kuoleana, kutembelea a na biashara, hivyo kutokana na Wazanzibar kuishiTanganyika na halikadhalika Watanganyika kuishi Zanzibar, suala la kuungana lilikuwa Kama liko tayari” alisema Balozi Lusinde. Aliongeza kusema kwamba baada ya Muungano, umoja, usalama na uchumi uliimarika. Balozi Lusinde alisisistiza suala la kuulinda na kuuimarisha Muungano wetu na kushauri changamoto zilizopo zizungumzwe na kutafutiwa ufumbuzi. Akizungumzia uwepo wa Serikali tatu, Balozi LUsinde alisema Hanoi haja ya kuwepo maana miaka 50, ya Muungano tunaona matunda yake.”serikali tatu hazina haja ya kuwepo, kwani zitaleta katika uendeshaji wake, pili serikali hizi zitakuwa na gharama ya uendeshaji wake, na tatu zitawachanganya wananchi” aliongeza Balozi Lusinde. Balozi Lusinde aliendelea kusema kwamba serikali tatu ni sawa sawa na kuweka gia ya kumrudi nyumbani kwenye gari na kwamba serikali tatu zitatupeleka kwenye uharibifu na kutusambaratisha. Balozi Lusinde alimalizia kwa kushauri kwamba Muungano wetu usiwekewe kitu chochote cha kuwavuruga Watanzania ili wasivurugike, wasitengane na wasigombane.

No comments:
Post a Comment