Baba wa
Lupita Nyong'o amesema maneno hayo wiki kadha baada ya Lupita Nyong'o
kupewa tuzo ya Oscar, Lupita ambae ni binti wa kikenya ambae alipewa
tuzo hio kwa umahiri wake alioonesha kwenye movie ya 12 YEARS A SLAVE,
Baba wa Muigizaji huyo amejitokeza na kueleza jinsi gani familia yake ilivyoteseka na kunyanyaswa nchini kenya.
Huku
Lupita akiwa anasifiwa na muongozaji wa Movie hio kuweza kuigiza
vipande vyake vizuri mpaka kufikia hatua ya kupewa tuzo, uigizaji wake
kwenye vipengele vya kusikitisha, ila familia yake pia walikua watu
wakuteswa, kunyanyaswa na pia kuuliwa.
![]() |
| Baba yake Lupita Nyong'o Mr Peter Anyang Nyong'o akiwa na binti yake Lupita wakati wa tuzo za Oscars |
kama
mpinzani wa aliekua Raisi wa Kenya Daniel Arap Moi, baba yake muigizaji
huyo, Peter Anyang Nyong'o ambae ni mwanasiasa nchini Kenya alikuwa
akiteswa mara kwa mara, huku mwili wa Mjomba yake Lupita aitwae Charles
Nyong'o haujaonekana mara baada ya mjomba huyo kuvamiwa akiwa feri na
kutupwa nje ya meli.
![]() |
| Lupita akifurahia mara baada ya kupewa tuzo hio ya Oscar |
Peter
Nyong'o, sasa ni kiongozi mwanasiasa anaetumikia kwenye seneti ya nchi,
ameeleza ukweli wa ndani walichokuwa wakifanyiwa, mpaka kuhamua
kukimbilia nchini Mexico ambapo Lupita alizaliwa mwezi Machi 1983.
Mr Nyong'o alieleza jinsi alivyo sumbuka kumwangalia mtoto wake akifanikiwa kwenye uigizaji.'Tuliwekwa Jela, kwenye machemba ya mateso, ila ilkua kama sherehe ya chakula cha usiku ukilinganisha na walichopitia watumwa,' mr Nyong'o aliiambia mtandao wa
Independent On Sunday
mr
Nyongo pia alisema kaka yake Charles alipotea mwaka 1980, miaka miwili
baada ya Moi kuwa raisi, na ndo wakati Mr Nyong'o akiongolewa kama mgumu
kwenye siasa.
Mwili wake haukupatikana na hakuna mtu aliepelekwa mbele ya haki kwa mauaji hayo.
'Hata
sasa, hakuna maelezo yaliotolewa kuhusu mauaji hayo. ninachokijua
alikua feri huko mombasa na shuhuda nilieweza kuongea nae alisema haikua
ajari ila alivamiwa na kusukumwa kutoka kwenye meli. Ila mashuhuda
walikua na uoga wa kueleza mbele ya polisi,' alisema Mr Nyong'o
Mr Nyong'o ana amini yakwamba kaka yake aliuliwa kutoka na upinzani wake na Mr Moi.
Wachunguzi wana amini kwamba Moi na watu wake walichukua hela za matumizi ya Kenyaa zaidi ya £3 billion katika miaka 24 yake ya Uongozi, na pia anajulika kwa jinsi alivyokuwa akitumia ulinzi wa nchi kuua na kutesa.
Mr
Nyong'o na mke wake walilazimika kuondoka kenya na kwenda Mexico,
alipopata kazi ya kuwa mwalimu wa Siasa ya kisayansi, na ndipo Lupita
alipo zaliwa.
Familia
yake ilirejea kenya 1987 ila walikua wakijificha kwenye nyumba za siri,
kwa sababu mr Nyong'o alikua akitengeneza chama cha siasa chini chini.
Akiwa
msichana mdogo Lupita pamoja na kaka na dada zake watano walitakiwa
kusafiri na wazazi wao kila mahali, huku baba yao akiwa anachuliwa na
polisi kila wiki, huku wanafamilia wengine wakiwa ni wakupigiwa simu za
vitisho kila siku.
![]() |
| Mr Nyong;o ambae ni mwanasiasa nchini Kenye anaamini kwamba kaka yake aliuliwa kwasababu ya upinzani wake na Raisi wazamani wa kenya Mr Daniel Arp Moi (Pichani) |
Mr
Nyong'o alifikia hatua ya kufikiri Lupita hayupo huru kwenye kukuza na
kuzingatia malengo yake, kuweza kumudu makazi mapya ilimsaidia kugeuza
malengo yake na kuwa muigizaji
Mr Nyong'o na Mke wake walisafiri kutoka Kenya kwenda kuhudhuria tuzo hizo za Oscar ambapo mtoto wake alichukua tuzo pia.
Alisema
"Lupita alinipigia na kuniambia alipochaguliwa kuwania tuzo hio.
Aliguswa sana kwa kuwa alifanya vizuri mpaka kuchaguliwa kuwania tuzo
hio.
![]() |
| Moja ya Vipengere alivyo igiza Lupita Nyong'o kwenye Movie ya 12 YEAR A SLAVE ambayo ilimuwezesha kupata Ushindi wa Tuzo za Oscar |
![]() |
| Lupita Nyong'o |





1 comment:
ukitoka na usemi huu unaula sana ukiwa majuu lakini chunguza ukikaa nao sana utaona hata hawakuthamini tena so be careful my dear sister be proud of your heritage, unadhani wazungu watakuthamini milele?
Post a Comment