Waziri anasema ‘Mshambuliaji alilitengeneza kwa kuchukua chupa ya Whisky iliyotumika na kuweka utambi na vitu vingine kisha mfuko wa plastick wenye misumari alafu akalitegesha
ndani ya Bar hiyo iliyokua imejaa watu wakitazama mpira saa mbili usiku’Unaambiwa kabla ya bomu kulipuka, alietegesha bomu hilo ambae mpaka sasa uchunguzi ukiendelea hajafahamika, alihamia kwenye Bar ya jirani iitwayo ‘Washington’ na kutegesha bomu jingine la kienyeji ambalo hata hivyo halikulipuka.
Wahudumu wa bar ya ‘Arusha night park’ wamesema wakati wa mlipuko huo waliona kwanza mwanga mkubwa na moshi kujaa ambapo wenzao wameumia sana ikiwemo kuvunjika miguu huku wateja baadhi wakiumia pia walipojaribu kukimbia kutoka kwenye eneo la tukio.
Hali ya sintofahamu iliyowakumba wakazi wa jiji la Arusha baada ya bomu kulipuka jana.
Majeruhi baada ya bomu kulipuka.
Mmoja wa maeruhi akiwa hoi baada ya mlipuko.
No comments:
Post a Comment