Mtanzania yeyote ambae anajua utaratibu wa usafirishaji kwenye nchi zilizoendelea kama South Africa, Uingereza na mataifa mengine duniani, anaweza kushawishika kutamani utaratibu huo ungekua unapatikana pia na nyumbani Tanzania.
Nilikua natazama TBC1 nikaona interview fupi ya Waziri wa uchukuzi Harrison Mwakyembe na nikafanikiwa kuipata akisema itajengwa reli nchini Tanzania kwa nguvu ya Uingereza baada ya kuona umuhimu wa matumizi ya reli kusafirisha mizigo na abiria ili kuepukana na yote yanayotokea barabarani.
Taarifa ilisema pia kuna mpango wa baadae wa kuleta treni za kisasa zinazotumia umeme ambazo zina sifa ya kufanya kazi kwa uharaka na uhakika kote duniani.
Una chochote cha kusema kuhusu hili?.
CREDIT:MILLARDAYO.COM
No comments:
Post a Comment