ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 28, 2014

DOCUMENTARY: TANZANIA; A JOURNEY WITHIN YAWAGUSA WENGI

 Washiriki wengi walijitokeza kuangalia documentatry hiyo ambayo tayari imeshajizoelea sifa tele, washiriki wengi  licha ya kuvutiwa ma maudhui yake  baadhi yao walijikuta wakitoa machozi baada ya kuguswa na  walichokiona
  washiriki wa onyesho wakiwa wamenyayua pipi  kijiti ambazo  ujumbe wake  ulikuwa  "Malaria Sucks" ikiwa ni ishara yao ya  kuunga  mkono  mapambano dhidi ya Malaria
 Wahusika wakuu wa Documentary  ambayo imetayarishwa nchini Tanzania,  wakijiandaa kujibu maswali, kutoka kushoto, Kristen Kennye,  Venance Ndibalema na  Bi,  Sylvia Caminer ambaye ndiye aliyeongaza decumentary hiyo, Sylvia ni mshindi wa  Tuzo kadhaa za Emmy.
Tangazo la onesho la Documentary : Tanzania;  a Journey within, kama  linavyoneka siku ya ufunguzi wake hapo April 25  jiji New York ,  siku ambayo Jumuiya ya Kimataifa ilikuwa ikiadhimisha siku ya Malaria Duniani. Kwa mujibu wa waandaji wa Documetary hiyo ambayo wahusika wake wakuu  ni dada wa Kimarekani   Kristen Kenney na kaka wa kitanzania, Venance Ndibalema mapato yatokanayo na  onesho la decumentary hiyo yanapelekwa kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa  malaria nchi Tanzania.

Na  Mwandishi Maalum
Documentary  Tanzania; A Journey Within, ambayo wahusika wake wakuu ni Kristen Keeney   dada wa kimarekani na  kaka  wa kitanzania Venance Ndibalema imekuwa kivutio kikubwa kwa watizamaji  wengi na kujizoelea sifa kemkem.
 Documentary hiyo imeanza  kuoneshwa katika baadhi ya kumbi za senema  hapa  jiji New York  Aprili 25 ambayo  ilikuwa Malaria   Duniani. Licha ya kuhudhuriwa na  watizamaji wengi mwandishi wa habari hizi ambaye alikuwapo siku ya ufunguzi alishuhudia namna watizamaji hao walivyoguswa  kiasi cha baadhi yao kutokwa machozi.

Ni documentary ambayo  inawakutanisha  wahusika wakuu  wenye mila na tamaduni zinatofautiana,  mmoja akitokea   katika  nchi iliyoendelea kwa kila kitu na  familia yenye uwezo na kijana  wa kitanzania  kutoka nchi  inayoendelea Tanzania.
Vijana hao wawili  urafiki wako ulianzia kwenye uwanja wa mpira, urafiki uliopelekea   kwa  Kristen kumshawishi Vencance aje kutembelea Tanzania,  na si kuishia katika  majiji na miji mikubwa ya Tanzania,  bali alitaka pia  kwenda vijijini  kujifunza na kama si kujionea maisha halisi ya mtanzania.
Ni  cocumentary ambayo   kwa  yeyote anayeitizima  hutoka akiwa mtu  mwingine na  nikra tofauti.  Documentary hii tofauti   na nyingine ambazo wahusika  huandikiwa mistari ya kukariri na maeneo ya kuingizia,  hii inaonyesha uhalisia wa si tu wawahusika wakuu bali,  maisha halisia ya mtanzania, ukarimu wao, upendo wao, raha zao, taabu zao, uvumilivu wao na kujituma kwao.
Ni maisha haya aliyoishi Kristen,  ambayo siyo tu yamembadilisha  mtizamo wake, lakini kwa  maneno yake anasema amezaliwa upya.
Akijibu maswali  mbalimbali kutoka  kwa watizamaji mwishoni mwa onesho ambalo  limeongozwa na mshindi wa tuzo kadhaa  za Emmy Award Sylivia Caminer.  Kristen ansema.
 “ Najijisi kuzaliwa  upya ,    upendo na ukarimu walionionyesha watanzania wale,  upendo wa kweli unaotoka moyoni, upendo ambao haukujali rangi yangu,  wala ninatoka wapi, umenitia moyo sana,  kiasi  cha kuona  kwamba kumbe mali na maisha mazuri bila ya upendo wa kweli hauna maana yoyote.
Kristen siyo tu alikwenda migombani na kukata mgomba wa ndizi na kuubeba kichwani,  kumenya ndizi,  kupika kwa kutumia kuni,  kuchota maji mtoni, mto ambao maji  hayo  hayo yalikuwa yakitumiwa na mfugo huku wengine wakioga, lakini pia alikuwa  mhanga wa malaria, ugonjwa uliomfanya alazwe kwa siku mbili na kupatiwa matibabu katika zahati moja   huko  Bukomba Vijiji.
Kuugua kwake  malaria, na upendo wake kwa watanzania na  kama  vile kurejesha fadhila, Kristine  na  mshirika wake wameamua kufanya  mambo mbalimbali ya kusaidia vita dhidi ya  malaria
Kwa mfano imeanzishwa  ijulikanayo kama  Malaika for life.   Asasi hii  hujishughulisha na uuzaji wa bangili,  urembo ambao  umetengenezwa  na wanawake wa kitanzania. Kauli mbiu ya  bangili  hizi ni  buy a bracelet, save a life. Kupitia mchango wa  Malaika for life,  michango hiyo imeweza kuokoa maisha  ya watu 22,000 dhidi ya   ugonjwa wa malaria.
Akiuguzumzia ugonjwa wa Malaria Kristen ambaye   licha ya kuishi maisha ya kijiji lakini  pia alipata fursa ya  kuupanda  Mlima Kimajaro hadi kileleni na vile vile kutembelea mbuga ya wanyama anasema, ugonjwa wa malaria unatibika.
“ Nimatumaini yetu kwamba  mnaponunua tiketi ya kuja kuangalia documentary hii  mnachangia katika  kuokoa maisha ya mtu  mmoja au mtoto mmoja michango  tunayopata tunanunua dawa pamoja na  vifaa vya kupimia  na kugundua ugonjwa wa malaria kwa  haraka na kwa muda mfupi” anasema Kristen
 Kwa upande wake,  Venance anasema  uamuzi wake wa kushiriki documentary hiyo ambayo itaonyeshwa hapa New York hadi   Mei mbili na baada hapo  itaonyeshwa katika majimbo mengine  likiwamo la Los Angeles.  Anaamini kwamba  utasaidia sana  kuokoa maisha ya watanzania wengi hususani  katika eneo hilo la  kupambana na  malaria.

No comments: