Advertisements

Sunday, April 13, 2014

IGP ATUMA TIMU MKOANI MARA db950-3

db950-3
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika siku za hivi karibuni, huko mkoani Mara wilaya ya Butiama kumejitokeza matukio ya mauaji yanayowalenga hasa akina mama wawapo katika shughuli zao mbalimbali.
Kufuatia matukio hayo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu ametuma timu maalum ya wataamu itakayoongozwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai nchini, DCI Issaya Mngulu kwenda mkoani humo kuongeza nguvu kwa kushirikiana na wataalam wa mkoa huo, ili kuhakikisha kwamba wote wanaojihusisha na vitendo hivyo wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria haraka.
Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi wanaoendelea kutoa ushirikiano utakaosaidia watuhumiwa hao kuendelea kukamatwa na linatoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Mara na maeneo ya jirani kuwa watulivu wakati upelelezi ukiendelea.
Aidha, Jeshi la Polisi nchini linawaomba wananchi wenye taarifa za wahalifu hao kutoa taarifa hizo kupitia namba za simu zifuatayo; 0715 009930, 0754 785557 au katika kituo chochote cha Polisi.
Imetolewa na:
Advera Senso -SSP
Msemaji wa jeshi la Polisi.

No comments: