ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 28, 2014

KILIMANJARO STARS NA ZANZIBAR HEROES WAFUNGANA 2-2 MKWAJU YA PENATI YALETA KIZAZAA

Mtanange wa Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes ulikua wenye upinzani mkali ambapo kipindi cha kwanza cha mchezo Kilimanjaro Stars walitawala mchezo na kuonekana kama wangeibuka washindi wa mechi hiyo iliyokuwa ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 50 ya Muungano iliyofanyika Juampili April 27, 2014 katika viwanja vya Greencastle Park, Fairland, Maryland na kuhudhuriwa na mashabiki lukuki wakiongozwa na wageni wa heshima Wazirii wa Nchi ya Ofisi ya Rais Zanzibar, Dr Mwinyihaji Makame na Naibu Waziri wa Fedha (S) Mhe. Mwigulu Nchemba wakiwa na mwenyeji wao Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula. Mpaka mapunziko Kilimanjaro Stars walikuwa mbele kwa goli 2-0

Kipindi cha pili mpira uligeuza kibao Zanzibar Heroes walishambulia muda wote wa mchezo na kuweza kusawazisha magoli yote. Mechi ilikua nzuri sana ispokuwa wachezaji wengi walilalamikia uwanja haukua wenye hadhi ya mechi ile pamoja na hilo kulitokea rabsha za hapa na pale laikini yote ilikuwa sehemu ya mchezo na burudani mapka dkk 90 magoli yalikua 2-2.

Ilipokuja mkwaju ya penati Kilimanjaro Stars walibadilisha kipa jambo ambalo lilipigiwa kelele na Zanzabar Heroes na baadae kukubali kupigiana panati. Kilimanjaro Stars ndio walioanza kupiga penati na walipata ya kwanza na Zanzibar Heroes na kuweka kmyani ya kwao, mkwaju wa pili Zanzibar Heroes wakaamua kubadilisha kipa na nafasi yake kuchukuliwa na kipa maaraufu Dedi Luba ambaye ndiye aliyesababisha penati kufikia kikomo baada ya kuipangua penati ya Lemmy Mhando na  Kilimanjaro Stars kusema alisogea mbele kabla ya penati kupigwa na refa kutopuliza kipenga. 

 Baadae Ubalozi ukaingili kati na kumaliza mzozo uliokuwepo kwa kusema lengo la mechi hii ni kuimarisha ushirikiano na kuleta mshikamano na upendo kati yetu na si kuleta utengano. Na baadae kukabidhi Kombe kwa Makepteni wa timu mbili na baada ya hapo wakalikabidhi kwa Mhe. Balozi Libarata Mulamula Awatunzie.
  Kilimanjaro Stars wanapata penati ya kwanza
 Zanzibar Heroes wanapata penati ya kwanza
 Zanzibar Heroes wamebadilisha kipa na kumuweka Dedi Luba hapa akiwa kwenye mstari wa goli.
 Hapa Dedi Luba anasogea mbele kabla ya penati kupigwa
 Hapa anapiga hatua nyingine tena kabla ya penati kupigwa
 Hapa aishafika mbele ya goli kabla penati kupigwa
 Mpira umepigwa Dedi Luba akiwa mbele ya goli
Dedi Luba amepangua penati
Kizazaa cha wachezaji wa pande zote kumzonga refa
Mashsbiki nao wameingilia kati
kwa picha zaidi bofya soma zaidi

1 comment:

Anonymous said...

dedi luba kama mteja na keshazeeka kwa nini wamemuweka na nani kashinda katika mechi hii tupeni habar habar moto moto vijimambo team thanks guys