Advertisements

Wednesday, April 16, 2014

MAFURIKO DAR ES SALAAM YAUA 41


Mafuriko yaliyotokea Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki yamesababisha vifo vya watu 41.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki alisema vifo 25 vimethibitishwa na ameagiza polisi kufanya uchunguzi zaidi kubaini watu wengine ambao hadi sasa hawaonekani waliko.
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa, eneo la Ilala, vilitokea vifo 11 ingawa inahisiwa watu wengine wawili hawaonekani. Kinondoni vifo ni saba huku wengine 14 wakidaiwa kuzikwa bila polisi kupata taarifa na Temeke vifo saba.
Sadiki alitaka uchunguzi wa
polisi ufanyike kila familia zilizokumbwa na msiba, hususani Kinondoni kuthibitisha kama vifo hivyo 14 vilitokana na mafuriko.
Kuhusu kurudi katika makazi yao kwa wakazi wa Jangwani alitaka watumie busara kwani kitendo hicho kinahatarisha maisha yao.
Alisema serikali haiwezi kubomoa nyumba husika kwani inasubiri uamuzi wa mahakama kutokana na kuwepo kwa kesi iliyofunguliwa dhidi yake

1 comment:

Anonymous said...

Viongozi wa Tanzania mnalea hili na oneni mnavyosababisha vifo ambavyo vingeepukika. Mnakua hela Bungeni na akumbano tu!!Kwa nini isiwepo sheria ya kutojenga mabondeni na kesi iliyofunguliwa mbona inakawia? Ila ya Babu Seya na Vyama vya upinzani sawa! Hamna sababu ya watu kufa maji enzi hii mnayongangania serikali mbili au tatu. Tuendeni na wakati acheni uzamani Zanzibar inavRais wake sivyo mfuteni!!!