Advertisements

Saturday, April 12, 2014

MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU MKOA WA NJOMBE‏

Baadhi ya wanafunzi wa shule zilizopo mkoa wa Njombe wakifurahia maadhimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika kimkoa katika wilaya ya Makete Aprili 11, 2014.
Mkuu wa wilaya ya Makete Mhe. Josephine Matiro akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kimkoa katika wilaya yake.
Mkuu wa mkoa wa Njombe kapteni mstaafu Aseri Msangi (Katikati) akipata maelezo kutoka kwa mwalimu aliyetunga vitabu kama njia mojawapo ya kuinua elimu mkoani humo, wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya makete Mh. Josephine Matiro na anayefuata na afisa elimu mkoa wa Njombe Bw. Said Nyasiro.
Wanafunzi wa sekondari nao wakiingia katika viwanja hivyo.
Kutoka kushoto mkuu wa wilaya ya Ludewa Mhe. Juma Madaha, Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Aseri Msangi, mkuu wa wilaya ya Makete Mhe. Josephine Matiro na Mkuu wa wilaya ya Njombe Mhe. Sara Dumba.
Mkuu wa mkoa akikabidhiwa risala kutoka kwa wanafunzi.
Afisa elimu mkoa wa Njombe Bw. Said Nyasiro akisoma taarifa ya elimu kimkoa.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Aseri Msangi akihutubia katika maadhimisho hayo.
Mkuu wa wilaya ya Makete akimpongeza mwalimu wa shule ya msingi kitulo kwa kupewa kikombe na Mkuu wa Mkoa baada ya shule hiyo kufanya vizuri katika mtihani wa taifa mwaka jana.
Kikundi cha SUMASESU kutoka Makete kikitumbuiza katika maadhimisho hayo.

No comments: