Mwigizaji Omotola Jalade-Ekeinde
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, mama huyo wa watoto wanne alisema kuwa kila mtu anaelewa heshima aliyokuwa nayo mbele ya jamii, hivyo haoni kama kuna umuhimu wowote wa kujipendekeza kwa wanasiasa au wafanyabiashara wakubwa.
BAADA ya kutajwa kuwa miongoni mwa mastaa wenye uhusiano na baadhi ya viongozi wa serikali hususani wanasiasa, mwigizaji Omotola Jalade-Ekeinde, ameibuka hadharani na kukanusha madai hayo.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, mama huyo wa watoto wanne alisema kuwa kila mtu anaelewa heshima aliyokuwa nayo mbele ya jamii, hivyo haoni kama kuna umuhimu wowote wa kujipendekeza kwa wanasiasa au wafanyabiashara wakubwa.
“Hivi karibuni waandishi kadhaa wa blog waliripoti kuwa kuna baadhi ya wasanii wakubwa wa Nollywood wamekuwa wakishirikiana na wanasiasa na viongozi wa ngazi za juu kutafuna pesa za serikali. Binafsi mimi Omotola sijawahi na sitawahi kufanya ujinga huo,” alisema.
“Hivyo msiniweke miongoni mwao tafadhalini, kwa muda mrefu nimekuwa nikijiweka mbali nao ili kuzidi kulipa hadhi jina langu.
“Kama wewe ni msanii na unataka kuwa na urafiki na wanasiasa si vibaya, lakini hakikisha urafiki wako unakuwa hauhusiani na masuala ya kazi.”
No comments:
Post a Comment