CCM TAWI LA UINGEREZA - UNITED KINGDOM
Website ccmuk.org, Blog ccmuk.org/blog, Facebook page chama cha mapinduzi uingereza, twitter CCMUK 1
Contacts Phone +44 74 04 863333, +44 7545 213515
E-mail - itikadi-uenezi@ccmuk.org
MAINA OWINO ANG'ATUKA UENYEKITI WA CCM TAWI LA UINGEREZA - UNITED KINGDOM
PIA HALMASHAURI KUU YA TAWI YAMSIMAMISHA KAZI
KATIBU WA TAWI BI. MARIAM MUNGULA
Mwenyekiti wa CCM UK Ndugu Maina Ang'iela Owino jana ametangaza rasmi nia yake ya kujiuzulu Uongozi wa CCM Tawi la UK baada ya kutumikia toka mwaka 2007.
Ndugu
Owino alitoa uamuzi huo wa hiari wakati akifungua rasmi kikao cha
Halmashauri Kuu ya CCM Tawi la UK kilichokaa jana Jumamosi tarehe
12/04/2014 katika jiji la Reading, Berkshire, Uingereza.
Ndugu Owino aliwakumbusha wajumbe kuwa awali aliomba kukitumikia Chama kwa muhula mmoja wa
uongozi na alitaja kumbukumbu ya vikao vya Chama vilivyomuomba aendelee kukisimamia Chama hasa baada ya kuchaguliwa viongozi wakuu wapya wa Tawi mwezi septemba 2012 jijini Manchester. Ndugu Owino aliwakumbusha mafanikio waliyopata katika muda wa uongozi wake ikijumuisha harakati za kufungua mashina hadi 15 katika miji na Jiji mbalimbali; Kuhamasisha na kujenga mtandao wa kuanzisha Jumuiya ya kwanza ya Watanzania hapa UK na Kuwashirikisha wanaCCM kuanzisha miradi ya kujitegema ikiwepo ari ya kumiliki jengo la CCM UK.
uongozi na alitaja kumbukumbu ya vikao vya Chama vilivyomuomba aendelee kukisimamia Chama hasa baada ya kuchaguliwa viongozi wakuu wapya wa Tawi mwezi septemba 2012 jijini Manchester. Ndugu Owino aliwakumbusha mafanikio waliyopata katika muda wa uongozi wake ikijumuisha harakati za kufungua mashina hadi 15 katika miji na Jiji mbalimbali; Kuhamasisha na kujenga mtandao wa kuanzisha Jumuiya ya kwanza ya Watanzania hapa UK na Kuwashirikisha wanaCCM kuanzisha miradi ya kujitegema ikiwepo ari ya kumiliki jengo la CCM UK.
Alikumbusha
pia juhudi na msukumo wa kutaka CCM Taifa kuanzisha dawati rasmi la
matawi ya nje na kuyapa uwakilishi wa kudumu katika vikao vya juu vya
CCM Taifa. Pia kupigania Sera ya CCM ya Diaspora iboreshwe kwa Kuanzisha
Kituo Maalum cha Diaspora nchini Tanzania ili serikali iwashirikishe na
kuratibu hoja na haja za wana Diaspora.
Aidha
aliwataka wajumbe kutoa ushirikiano wa wazi kwa Idara ya uenezi ambayo
kwa sasa inajenga Website ya kisasa na Online TV itakayowapa wanaCCM
uhuru wa kutoa maoni na hoja zao bila uwoga lakini kwa nidhamu na
kufungua soko la kutangaza bidhaa za Tanzania.
Ndugu
Owino alisema wanaCCM hujenga umoja wa kweli na hawaogopi kusingiziwa
au kusemwa vibaya na hivyo wasiogope changamoto mbalimbali wakati
wanatekeleza Mapinduzi ya umma na kukijenga Chama hapa Uingereza.
Ndugu
Owino aliiomba Halmashauri Kuu ya Tawi ishirikiane na Sekretariati ya
Halmashauri Kuu ya Tawi kufanya maandalizi na kupanga tarehe ya Mkutano
Mkuu wakati wowote kuanzia sasa ili wanaCCM wote wawe huru kumchagua
kiongozi atakaye sukuma CCM UK toka hapa tulipofikia.
Wakati huohuo Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi la UK jana iliazimia kwa pamoja kumsimamisha Katibu wake wa Tawi Mariam Mungula baada
ya majadiliano ya kina ya kutokuridhishwa kabisa na utendaji na uratibu
wake wa kazi. Kikao hicho kilipeleka shauri lake kwa Kamati ya Maadili
na Usalama ili apate haki ya kujitetea ni kwa nini asiachishwe moja kwa
moja kazi yake za Ukatibu wa CCM UK. Ndugu Leybab Mdegela anakaimu nafasi yake kuanzia jana 12/04/2014.
Kikao
kiliendelea na hoja zake za kuboresha Chama hapa UK na kuweka mikakati
yenye mawazo chanya katika kukisaidia chama katika mikakati kuleta
maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wote wa Tanzania.
Imetolewa na Abraham Sangiwa
Idara ya Itikadi na Uenezi ya Halmashauri Kuu ya CCM UK.
13/04/2014.
1 comment:
If anyone can educate me on the benefits of these CCM/Chadema/Cuf branches et al in Ulaya, Marekani etc, I will join one tomorrow. I really don't get it. Where do people get the time and do those countries allow its Citizens to get involved in such bizzare politics? "god" bless you all.
Post a Comment