Advertisements

Sunday, April 13, 2014

Taarifa ya Polisi kuhusu idadi ya waliofariki Dar kutokana na hizi mvua.


06m 
Kutokana na mvua zinazonyesha hivi sasa kwenye jiji la Dar es salaam pamoja na kusababisha mambo mengi kusimama, miundombinu kuharibika hasa madaraja yanayounganisha njia kuu, pia zimesababisha vifo vya watu 10.
Nyumba nyingi zimeingia maji hasa
maeneo ya mabondeni na kulazimisha familia kuhama kutoka kwenye makazi yao ambapo mpaka sasa Polisi Dar es salaam inasema  watu kumi waliofariki, wamo watoto watano na watu wazima watano.
Kamanda Suleiman Kova wa kanda maalum ya Dar es salaam amesisitiza hali sio nzuri hivyo wananchi wanatakiwa wachuke tahadhari kwenye makazi yao na hata wanaotembea na magari barabarani kwa sababu njia nyingi zina mashimo na pia watu wapunguze mizunguko isiyo lazima barabarani.
Hizi ni baadhi ya picha kati ya nyingi zinazosambaa kwenye mtandao.
3
4
5
6


No comments: