Thursday, May 29, 2014

CHAZ BABA: SAJENT HAKUSTAHILI KUOLEWA NA MIMI

RAIS wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ amefunguka kuwa mwigizaji Husna Idd ‘Sajent’ hakustahili kuwa mkewe licha ya kwamba walizaa naye mtoto mmoja.
Akizungumza na Global TV Online hivi karibuni, Chaz Baba alisema Sajent ni mwanamke mzuri lakini hana vigezo vya kuolewa na yeye kwani wote ni maarufu.
Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ akizungumza na Global TV Online.
“Nilikuwa nampenda sana Sajent ila nilishindwa kumuoa kutokana na umaarufu wake ambao ulimnyima sifa ya kuolewa na mimi maana wote ni mastaa ingekuwa shida huko mbeleni,” alisema Chaz Baba.
Mbali na hilo, Chaz alifunguka mengi ambayo yatarushwa kupitia.
GPL

5 comments:

Anonymous said...

Huyu jamaa inaelekea hajiamini kama mwanaume. Inaelekea anatafuta mwanamke ili yeye ndio amtawale!

Anonymous said...

kwa hiyo ulifuata uroda? kazi kuaribu au kuwachezea watoto wa wenzenu!!! kama ulijua hilo kwa nini ulimfuata !!! just keep you mouth shut!!!!

Anonymous said...

Jamaa huyu ni BOMU ana umaarufu gani mpaka anaanza kuongea ovyo hivi. DJ Luke jaribu kuwa mwangalifu posting kama hii haina maana ni kujenga chuki tuu na dada zetu, Kwani umaarufu ndio unaoa au watu wenyewe.Jamaa anahitaji PSYCHOLOGIST amsaidie.

Anonymous said...

na si huyu tu peke wanaume wengi tu mwanamke akiwa maarufu au msomi au anapesa kuliko yeye basi huwa mwanamme anakuwa kama uyoga huwa wanapenda sana mwanamke awe chini na wao wawe juu yao katika karne hii ya 21 century mbona wanaume kama hawa watatoka patupu because wanawake siku hizi moto moto wanajituma ile mbaya na wako fresh ile mbaya.kalaga baooooo wanaume kama huyu

Anonymous said...

Huyu jamaa si mjinga wala mpumbavu ILA ameona mbali...heri nusu Shari kuliko shari kamili...vigezo vya umaarufu , pesa, usomi na uzuri si vigezo sahihi vya kumtafuta mwanamke wa Kuoa...otherwise itakula kwako..