ANGALIA LIVE NEWS
Saturday, May 31, 2014
MISA YA KUMUAGA MWESIGA BLANDESI, OAKLAND, CA
Familia ya Mwesigwa inapenda kuwataarifu kuwa kutakuwa na misa ya kumuaga mpendwa wao Mwesigwa Blandesi itakayofanyika siku ya Jumamosi May 31,2014 kuanzia saa Nane na nusu mchana mpaka saa kumi na moja na nusu jioni(2:30-5:30pm) katika Kanisa la "Resurrection Lutheran Church", 397 Euclid Avenue, Oakland California 94610.
Baada ya misa kutakuwa na mkusanyiko wa ndugu jamaa na marafiki wote kwenye ukumbi wa "Resurrection Lutheran Church" katika kusheherekea maisha na kumbukumbu ya marehemu Ndugu Mwesigwa Blandesi. Tafadhali sana tuzingatie muda wa Ibada.
Ndugu yetu Mwesigwa Blandesi alifariki tarehe 26/5/2014 baada ya kuugua kwa muda mrefu kwa ugonjwa wa Saratani na anatarajiwa kusafirishwa kwenda nyumbani Tanzania. Marehemu ameacha Mke na watoto wanne.
"Mwenyenzi Mungu aiweke mahali pema roho yake, Amen".
Michango yenu ya hali na mali bado inahitajika katika kufanikisha maandalizi ya kumsafirisha Marehemu pamoja na mipango yote ya mazishi. Tunatanguliza shukrani zetu za dhati.
Ile harambee ya kuwachangia familia ya Marehemu itafanyika leo siku ya Jumatano tarehe 28/5/2014 nyumbani kwa marehemu, 4093 Memoir Avenue, Tracy, California 95377 kuanzia saa moja na nusu jioni.
Kwa wale ambao watashindwa kufika au wapo mbali naomba tupeleke rambirambi zetu kupitia kwenye akaunti namba ifuatayo:
Bank of America
Bank Account Number : 002542068968
Jina: Rosemary Byorwango
Kwa taarifa zaidi unaweza kuwasiliana na wafuatao:
Erick Byorwango ( 510 520 5995)
Josephene Masabala (510 484 5085)
Dr. M. Kaaya (510 290 9708)
Kiongozi yeyote wa TCO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment