Saturday, May 31, 2014

MZEE MZIMBA AICHANA YANGA LIVE

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kundi la Yanga Asili Yusufu Mzimba 
Mzimba hakuishia hapo, amesisitiza kwamba Yanga haiwezi kuwa kampuni hata siku moja na ikitokea hivyo basi kampuni hiyo ni lazima itakufa.
YUSUPH Mzimba aliyekuwa Mwenyekiti wa Kundi la Yanga Asili ameibuka kutoka mafichoni na leo Jumamosi ataonekana makao makuu ya Yanga kuomba taarifa za maendeleo ya klabu kabla ya kesho Jumapili kuibuka katika mkutano mkuu wa marekebisho ya Katiba.


Mzimba hakuishia hapo, amesisitiza kwamba Yanga haiwezi kuwa kampuni hata siku moja na ikitokea hivyo basi kampuni hiyo ni lazima itakufa.


Katika mahojiano maalumu yaliyofanyika jana Ijumaa, Mzimba anayeonekana kuzeeka zaidi, aliliambia Mwanaspoti kuwa hajapata taarifa za Yanga kwa muda mrefu, hivyo analazimika kutumia muda wake leo Jumamosi kufika klabuni hapo huku akidai kuwa yale yote ambayo hayapo sawa atayapiga chini.


“Nilikuwa kimya kwa miaka mingi kwa sababu zangu binafsi, nilikuwa nafanya mambo yangu lakini huku nikifuatilia mwenendo wa Yanga, nalazimika Jumamosi kwenda klabuni kupata taarifa kamili kutoka kwa viongozi wa Yanga.


“Nikipita taarifa hizo nitazitolea uamuzi hapo hapo na sitakwepesha ukweli, yale ambayo yatakuwa mazuri kwa maendeleo ya klabu yatatakiwa kuachwa kama yalivyo lakini yale ambayo ni kinyume nitawaambia wayaondoe mara moja,” alisema Mzimba.


Suala la Yanga kuwa kampuni ambalo alikuwa anapingana nalo tangu miaka ya nyuma, Mzimba alisema “Haitatokea hata siku moja Yanga ikawa kampuni na ikitokea hivyo basi ni lazima itakufa tu haiwezi kuendelea, Yanga ni ya wananchi na ikiwa kampuni itakuwa ya mtu binafsi jambo ambalo sikubaliani nalo.


“Kama wanataka kuwepo na kampuni basi Yanga waiache kama ilivyo ila wanaweza kufungua kampuni ndani ya Yanga, wafungue kampuni hata 10 lakini Yanga ibaki kuwa mali ya wananchi,” alisema na kusisitiza kuwa msimamo huo hauwezi kubadilika kamwe.


Miaka ya nyuma kulikuwepo na mgogoro mkubwa kati ya Yanga Asili na Yanga Kampuni kuhusiana na suala hilo ambalo baadaye lilishindikana kwa makubaliano kuwa Yanga ibaki kuwa klabu ya

No comments: