Saturday, May 31, 2014

MAPENZI YAITEKA DUNIA KILA KUKICHA MALA HILI MALA LILE JUU YA MAPENZI

Msanii wa Bongo Muvi, Rose Ndauka.

Wiki iliyopita katika Exclusive Interview tuliona sehemu ya kwanza ya Rose Ndauka alivyoeleza kuwa aliwamwaga wanaume na kutulia na Maliki. Wawili hao kwa sasa wanaogelea katika penzi zito na mikakati thabiti ya ndoa imeshaanza, wanatarajia kuoana baadaye mwaka huu.
Leo tunaendelea, atafungukia skendo za kupora waume za watu.
Risasi: Kuna taarifa zilienea kuwa uliwahi kutoka na baba mtoto wa Snura Mushi (mama Majanga), kuna ukweli wowote?
Rose: Nilishawahi kusikia skendo hiyo lakini aliyekuwa anadhania hivyo ni Snura, hakujua tu kama yule alikuwa ni mshkaji wangu na mimi nilimjua Snura walipokuwa kwenye uhusiano.
Risasi: Mbali na huyo, mbona inatajwa kuwa uliwahi kumnyang’anya mwigizaji mwenzio, Yvone Cherry ‘Monalisa’ mpenzi wake? Tena inasemekana mlikuwa marafiki!
Rose Ndauka akiwa na mume wake Maliki.

Rose: Sijawahi kuwa na urafiki na Mona (Monalisa) na huyo aliyezua hayo maneno ni Richard, siyo kweli kwani tuliwasiliana kawaida yeye akapindisha maelezo, shahidi ni baba mtoto wangu aliyeunganishwa na baba mtoto wangu pamoja na marehemu Kanumba (Steven).

Risasi: Umekuwa ukihusishwa na uvutaji wa bangi mara kwa mara, unalizungumziaje hilo?
Rose: Sijawahi kuvuta bangi ila nimewahi kunywa pombe sana hasa nilipokuwa na ‘stress’ na yote niliyokuwa nayafanya mwisho wa siku nilikuwa nikiyajutia.

Risasi: Ni kitu gani kilikufanya ujutie hasa katika suala zima la kugida ulabu?
Rose: Kuna habari imewahi kutoka gazetini nikiwa nabusiana na Maya, iliniumiza sana kwani tulitafsiriwa vibaya kwenye jamii na haitakuja kufutika kwani nilifanya matendo yale kwa sababu ya pombe na toka siku hiyo kiukweli niliacha unywaji wa pombe za vile, nilijuta.

Risasi: Ukipata nafasi ya kuongea na wasichana wasagaji utawaambia nini?
Rose Ndauka: Nitawashauri kuacha kabisa mambo hayo kwani ni ya kuiga tu, wajisomee vitabu vya kila aina ili kujinusuru kwenye tatizo hilo hasa vyenye mafunzo na kuonesha madhara ya usagaji.
Risasi: Tunafahamu kwamba mumeo mtarajiwa umemkuta na mtoto, unamleaje na hujawahi kupata malalamiko kama mama wa kambo?

Rose: Mimi ni kipenzi cha watoto, nampenda na yeye ananipenda, ninapomuona ana kosa namuadhibu kama mwanangu na sitarajii mtu kunisema vibaya kwani malezi ninayompa ni mazuri kama ambavyo namlea wa kwangu.
CREDIT:GPL

No comments: