Saturday, May 31, 2014

MOROGORO yamuaga GEOGRE TYSON, Sasa ni msafara wa kuelekea Dar es Salaam

Msanii wa Bongo Fleva AY akiwa amewasili na crew yake nzima kuja kumpa pole Mbonie Masimba, AY alitoa laki 6 kununua jeneza la marehemu Tyson hii ikiwa kama mchango wake kwa kuthamini kile alichomfania wakati akiwa hai. Sasa msafara unaelekea Bongo na mwili utafikia Hospital ya Kairuki iliyopo Mikocheni na naambiwa msiba uko upo Bahari Beach nyumbani kwa marehemu.
Wasanii na watu mbalimbali waliofika kuaga mwili wa George Tyson aliyefariki usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya gari Morogoro baada ya gari alilokuwa akiendesha marehemu kuacha njia na kupinduka huku likibingilika mara tatu ndani ya gari hilo pamoja na abiria wengine kuwepo kiti cha nyuma alikuwemo MC maarufu Gladys Chiduo maarufu kwa jina la MC Zipopamba aliyekuwa amekaa kiti cha mbele na amesema kilichomuokoa yeye ni kufunga mkanda.
Wasanii na watu mbalimbali wakiwa kwenye mstari wa kuaga mwili wa marehemu George Tyson.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Picha kwa hisani ya Dj Choka Blog

No comments: