Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia maharage mabichi
yaliovunwa kutoka kwenye shamba la kampuni ya kilimo ya Singida ambao
wanalima kwa kisasa umwagiliaje wa matone, kulia kwake anayempa
maelekezo ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo ya kilimo Ally Mohamed.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdukrahman Kinana akiangalia bomba nyembamba
zinazotomuka kumwagilia kwa matone kwenye shamba la kampuni ya kilimo ya
Singida .
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kuandaa shamba katika
shamba la maharage mabichi wilayani Ikungi mkoa wa Singida, shamaba hilo
la kisasa ni mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa matone ambalo lipo
chini ya Kampuni ya Kilimo ya Singinda (Singida Agriculture .co.ltd)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
wakishiriki kuweka maharage mabichi kwenye boksi tayari kwa
kusafirishwa kwenda kwenye masoko,Maharage hayo yanalimwa kwa kilimo cha
kisasa cha umwagiliaji wa matone mkoani Singida.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi madaftari kwa watoto
wanaoishi kwenye mazingira magumu yaliyotolewa na umoja wa akina mama wa
CCM wilaya ya Ikungi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wilayani Ikungi, Singida.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa darasa la shule ya msingi Unyaghumpi katika Jimbo la Singida Mashariki.
Wanafunzi wa awali shule ya msingi Unyaghumpi
katika Jimbo la Singida Mashariki wakiwa wamekaa chini kwa kukosa
madawati darasani, hii shule ipo kwenye jimbo la Mbunge Tundu Lissu
ambaye inasemekana amezuia wananchi wake wasichangie kwenye miradi ya
maendeleo.
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisaidia kuvuna mtama na uwele kwenye
shamba bibi mjane asiye na mtoto, Mayasa Mkhandi katika Kata ya
Unyaghumpi, Jimbo la Singida Mashariki, mkoani Singida,wakati wa ziara
yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi
wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya
CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza
kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mlezi
wa Mkoa wa Singida na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Ndugu Hadija Aboud
akishiriki kuvuna mtama na uwele ,Ikungi mkoani Singida.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye eneo la mkutano wa hadhara katika tarafa ya Mungaa, Makiungu
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara
ulofanyika katika Kijiji cha Makiungu, wilayani Ikingu, Jimbo la
Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu wa Chadema. Katibu Mkuu wa CCM
aliwataka wananchi hao wafikirie zaidi kuhusu maendeleo ya jimbo lao na
kuacha kuamini maneno ya viongozi wao wanaowazuia kuchangia maendeleo ya jimbo lao.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnaye akihutubia wakazi wa Makiungu, tarafa ya Mungaa na kuwaambia wananchi hao wakati umefika wa kuwaomndoa viongozi ambao wanawazuia wananchi kuchangia maendeleo yao.
Aliyekuwa
kiongozi wa Chadema, Ismail Gwau, akitupilia mbali bendera ya CHADEMA
mara baada ya kutangaza kujiunga na chama cha CCM,katika Mkutano huo wa
hadhara.
Ismail Gwau, akionyesha kadi mpya ya CCM mbele ya Kinana na kuashiria kujiunga rasmi na CCM,Ikungi mjini.
Wananchi wa Ikungi mjini wakila kiapo cha CCM.
No comments:
Post a Comment