Sunday, June 1, 2014

CHADEMA yapata msaada wa mil 700/= kutoka Denmark

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesaini mkataba wa Sh milioni 700 na Conservative Peoples Party cha Denmark.

Hayo yalisemwa juzi na Katibu Mtendaji katika Ofisi ya Katibu Mkuu, Victor Kimesera, wakati wa kutia saini mkataba huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

“Tunawashukuru sana kwa mchango huu tunaamini utaweza kuwasaidia akina mama wengi na vijana ambao wameonekana kuwa nyuma katika siasa ili na wao wawe na uwezo kisiasa,” alisema Kimesera. --- via Ziro99 blog.

No comments: