ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 1, 2014

Homa ya dengue yazaa operesheni itakayotoza faini papo kwa hapo kwa nyumba, shule Dar

Wafanyakazi wa Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Manispaa za Dar es Salaam, wataanza kampeni ya kukagua maeneo ya makazi ya watu yenye vichaka vinavyofanya mbu wa kueneza ugonjwa wa homa ya dengue, kuzaliana.

Watu hao watatozwa faini za papo hapo na nyumba zao zitafanyiwa usafi.

Akizungumza na mwandishi wa HABARI LEO juzi, Ofisa Ufuatiliaji wa Magonjwa wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alex Mkamba alisema kampeni hiyo inaanza hivi karibuni kwa kufanya ukaguzi katika makazi ya watu na shule, lengo ikiwa ni kukabiliana na homa ya dengue.
“Tunaanza kampeni ya kukagua maeneo ya watu, ambayo hayajafanyiwa usafi yanayosababisha mbu kuzaliana na tutashirikiana na Manispaa zote za jiji,” 
alisema Mkamba na kuongeza kuwa watatoza faini shule ambazo hazijatoa elimu kwa wanafunzi wao juu ya homa ya dengue.

No comments: