ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 17, 2014

GARI YA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA SHINYANGA YAPATA AJALI MBAYA MJINI KAHAMA


 
Gari hilo likiwa eneo la tukio baada ya kuangua na kuharibika vibaya.
Gari la Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, yenye namba T 862 BBC aina ya JEEP, imepata ajali jana mchana katika maeneo ya Nyasubi Kahama, kwenye barabara kuu iendayo nchi jirani za Rwanda na Burundi.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio, mara baada ya ajali hiyo dereva wa gari hilo  ambaye hajafahamika mara moja alikimbia, huku ikiarifiwa kuwa alipata majeraha kidogo kwani gari liliangukia upande wake.



Mtu mwingine ambaye alikuwepo katika ajali hiyo hakupata majeraha yoyote, na kwamba Gari hiyo imeinuliwa na kuondolewa eneo la tukio.

Akizungumza   kwa njia ya simu Mwenyekiti huyo wa ccm mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja amesema yeye hakuwemo katika gari hilo

Gari hiyo muda mfupi baada ya kuinuliwa kutoka mtaroni


 
Credit: na Malunde1 blog

No comments: