“Kama unakumbuka niliporudi hapa mambo hayakwenda sawa kila nilipowasiliana nao kule. Nilipokuwa kule, naona kuna vitu nilipoteza katika kiwango changu, lakini nashukuru baada ya kuitwa Taifa Stars nimerudisha kitu na kuwa katika kiwango changu cha kawaida ingawa siyo sana.”
Kapombe amesajiliwa na Azam FC kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea AS Cannes inayoshiriki Ligi Daraja la Nne Ufaransa ambayo ilimnunua kutoka Simba.
Katika mahojiano na Azam TV, Kapombe alisema: “Napenda kucheza mpira nje ya nchi, lakini kilichonirudisha ni matatizo yangu na klabu niliyokuwa nacheza kule. Niliposhauriana na washauri wangu, waliniambia nitafute timu inayonifaa hapa nchini ili niboreshe kiwango changu.
“Kama unakumbuka niliporudi hapa mambo hayakwenda sawa kila nilipowasiliana nao kule. Nilipokuwa kule, naona kuna vitu nilipoteza katika kiwango changu, lakini nashukuru baada ya kuitwa Taifa Stars nimerudisha kitu na kuwa katika kiwango changu cha kawaida ingawa siyo sana.”
Kapombe alikwenda mbali na kuweka wazi sababu iliyomfanya achague kujiunga na Azam akisema anaamini itamsaidia kukamilisha malengo yake. Pia alisema amevutiwa na klabu hiyo iliyojitosheleza kwa kuwa na vifaa vyote vya michezo kama uwanja na gym.
“Azam kuna kila kitu, lakini pia nimependa changamoto iliyopo hapa kati ya wachezaji na wachezaji,” alisema.
No comments:
Post a Comment