ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 23, 2014

Kondomu zakutwa kwenye ukumbi wa bunge

Kwa ufupi
Kutokana na sintofahamu hiyo Spika Alex Ole Magelo aliwataka wahudumu kufungua boksi hilo kujua kilichomo ndani yake ndipo walipokuta kondomu.
Nairobi, Kenya. Inaweza kuonekana ni kituko cha aina yake, lakini ni kweli kimetokea kwenye Ukumbi wa Bunge la Kaunti ya Nairobi na kuwaacha wabunge vinywa wazi.
Katika hali isiyo ya kawaida, boksi la kondomu lilikutwa ndani ya ukumbi huo na kuwashtua wabunge wote akiwamo spika wa bunge hilo.
Mwakilishi wa eneo la Karura, Kamau Thuo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuliona boksi hilo na kuwashtua wabunge wengine hali iliyoibua mjadala mzito.
Kutokana na sintofahamu hiyo Spika Alex Ole Magelo aliwataka wahudumu kufungua boksi hilo kujua kilichomo ndani yake ndipo walipokuta kondomu.
“Nafahamu wote humu ni watu wazima, lakini
ninachoshangaa ni nani ambaye ameleta kondomu hizi ndani ya ukumbi huu,” alihoji Spika Magelo.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Afya, Manoah Mboku aliwaondoa hofu wabunge na kueleza kuwa kondomu hizo zilipaswa kuwekwa kwenye vyoo vya wanaume hata hivyo kwa bahati mbaya zikapelekwa mahali kusikohusika.

No comments: