Naomba msaada tafadhali sana.
M-Pesa yarejea hewani
· Tatizo la kiufundi latatuliwa.
· Wateja waombwa radhi, waendelea kuituminia
Dar es Salaam, Tanzania June 18, 2014: Wateja
wa huduma ya M-pesa wamehakikishiwa usalama wa fedha zao wakati ambapo
huduma hiyo ikiwa imerejea kwa asilimia mia moja baada ya kukosekana
kufuatia tatizo la kiufundi lililojitokeza mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Vodacom Tanzania Rene Meza amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es
salaam leo kuwa huduma hiyo kwa sasa iko imara na kuchukua nafasi hiyo
kuwoamba radhi wateja kwa usumbufu walioupata wakati huduma hiyo
ilipokosekana.
“Napenda kuwaomba radhi
wateja wetu ambao wamekuwa na wakati mgumu kupata huduma ya M-pesa
katika siku chache zilizopita. Tunatambua umuhimu wa huduma hii kwao.
Hali iliyojitokeza ilikuwa nje ya uwezo wetu na kamwe
hatukulitarajia.”Alisema Meza
Meza amesema kilichotokea
kwenye mfumo wa M-pesa ni changamoto ambayo mfumo wowote unaotumia
teknolojia unaweza kukumbana nayo bila kutarajia lakini jambo la muhimu
ni kwa jinsi gani mtoa huduma anavyoweza kujipanga kuitatua kwa uharaka
kudhibiti madhara makubwa zaidi kwa wateja.
“Unapokuwa katika suala la
teknolojia chochote kinaweza kutokea ni kama vile inavyoweza kutokea
kompyuta kukataa kuwaka lakini cha msingi ni kwa uharaka gani unaweza
kudhibiti tatizo na kufikia ufumbuzi, hilo ndilo tulilolifanya na kwa
sasa tunayo furaha kwamba wateja wetu wanaendelea kupata
huduma.”Aliongeza
Kuhusu usalama wa fedha
Meza amewahakikishia wateja wa Vodacom na wabia wake wote wanaoutumia
huduma hiyo kwamba fedha zote zipo salama na zinalindwa kwani
kilichotokea ni wateja kushindwa kuipata huduma hiyo kwenye menyu za
simu zao za mkononi na sio tatizo kwenye mfumo mzima wa M-pesa.
‘Fedha zote zipo salama na
zinalindwa. Kama wakati tatizo lilipotokea mteja alikuwa na Sh 1/- au
Sh 100/- ,Milioni basi ni kiwango hichohicho atakuwa amekikuta kwenye
akaanti yake ya M-pesa au hata ya M-pawa mara baada ya huduma
kurejea.”Alifafanua Meza
Meza amewashukuru wateja
wa M-pesa kwa uvumilivu na ustahamilivu wao wakati timu ya watalaamu wa
ndani na nje ya nchi walipokuwa katika juhudi za kutafuta uvumbuzi wa
tatizo lililojitokeza.
“Wateja wetu wamekuwa
wavumilivu na wameendelea kuitumia kupitia mawakala zaidi ya 70,000
walioko nchi nzima. Hili unaweza ukaliona kupitia namna ambavyo wateja
walivyoendelea kuitumia M-pesa mara baada ya kurejea, tunawashukuru sana
na tunaendelea kuwaahidi huduma bora.”Aliongeza
“Hakuna madhara ya
kibiashara kwetu, ila kutokana na M-pesa kuwa tegemezi kwa mamilioni ya
watanzania katika maisha yao ya kila siku ikiwa ndio huduma kinara ya
fedha kwa njia ya simu za mkononi, ni wazi kwamba imeleta usumbufu
mkubwa kwa watumiaji.”
No comments:
Post a Comment