Advertisements

Wednesday, June 18, 2014

RAILA AZUNGUMZIA SAKATA LA LAMU




Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesema matamshi ya Rais Uhuru Kenyatta kuhusiana na
mashambulio ya Mpeketoni kuwa yamechochewa kisiasa, ni jambo la kukurupuka na linaweza kuathiri uchunguzi unaoendelea.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Nairobi, Bw Odinga amesema ni makosa kuhusisha siasa na mikutano yake ya hadhara ambayo amekuwa akiifanya, na mashambulio ya Lamu.
Amesema muungano wa chama chake hauna nia ya kuiondoa serikali iliyopo madarakani, na kuwa wataendelea na mikutano yao kuishinikiza serikali kuwa na mjadala wa kitaifa.

No comments: