Liban Newa alizaliwa huko Nairobi mwaka 1969 na kuhamia Dar es Salaam mwka 1977...Alianza kucheza Golf akiwa na miaka 13 katika Club ya michezo ya Gymkhana...
Liban mshindi wa 1987 Tanzania Safari Open Golf Championship. Hapa alipewa kombe na Balozo Ali Hassan Diria (marehemu) na Mr Haji mmiliki wa CMC Landrover Tanzania
Alianza na Handycap 13 mpaka akafikia Handycap 1...Newa pia alikuwa anapenda kucheza mchezo wa Squash...
Liban akipokea zawadi ya Best Gross ya Chairman's Trophy
Wakati anacheza Golf aliwahi kuwakilisha Tanzania kwenye michuano mingine Dubai, Uganda, Kenya na South Africa...Ameshinda vikombe vingi sana na ilipofika mwaka 1993 alikuwa Professional Golfer na akaanza kufundisha Golf hapo Gymkhana Club...
Liban Newa akiwa na timu ya Golf ya Tanzania njiani kuelekea Dubai kwa michuano 1993
Baada ya kuwa Pro aliwkilisha Tanzania kwenye mashindano mengi tu huko Kenya na Zimbabwe...Mwaka 1996 aliamua kwenda Marekani kuendeleza kipji chake cha Golf...Huko Marekani yuko kwenye Golf Galaxy Tour ambayo anacheza akiwa na Handycap 1...
Sasa anaishi North Carolina na mara kwa mara huwa anarudi nyumbani kucheza Golf...Anatrajia kurudi na kusaidia Golf ikue hapa Taanzania kwa kufundisha vijana na watu wengengine wenye mwamko wa Golf...
Safi sana Liban Newa kwa kutuwakilisha vyema huko Marekani...Max Sports inakukaribisha sana Tanzania...Max Sportsinapenda kuwakumbuka vijana wanaofanya vyema kwenye michezo popote walipo...





2 comments:
Congratulations Uncle Liban. Very proud of you.
Da Alu and Uncle Julius
Congratulations Liban,
I'm so proud of your great achievements.Growing up with you and seeing how hard you worked and how much you loved Golf, yes you do deserve recognition! Hard work really pays off!
All the best,
Tuma
Post a Comment