Waandishi wa
habari, Hamida Shariff (Mwananchi) (kushoto)Agnes Haule Habari Leo
(Kulia) na Askari Polisi (wa kati) kwa pamoja walishindwa kutimiza
majukumu yao na kuangua vilio kwa uchungu baada ya mwili wa mtoto Nasra
kuwasili Mochwari ya mkoa wa Morogoro
Ukiingizwa Mochwari
Ukihifadhiwa kwenye jokofu
Mapaparazi wa vyombo mbali mbali vya habari wakichukua tukio hilo
Bi. Josephine Joel ambaye alijitolea kumuuguza mtoto Nasra akimlilia mwanae
Bi Josephine akihojiwa na waandishi wa habari
Afisia Ustawi
wa Jamii mkoa wa Morogoro Bw Oswad Ngungamtitu akizungumza na waandishi
wa habari baada ya kuwasili kutoka Dar muda mfupi uliopita
Baba Mazazi
wa Nasra Bw Rashid Mvungi ambaye yuko nje kwa dhamani akiwa juu ya gari
baada ya kurejea kutoka jijini Dar alikoenda kuuchukua mwili wa marehemu
Nasra
Baba huyo wa Nasra akiwa na huzuni kubwa.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
MWILI wa marehmu Nasra Mvungi umewasili muda huu majira ya saa 10 na
dakika 2 mkoani hapa ukitoka hospital ya taifa Muhimbili jijini Dar es
salaama.
Baada ya
msafara huo uliongozwa na Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro Bw
Oswad Ngungamtitu kuwasili kwenye chumba cha kuhifadhia maiti hospital
ya Rufaa mkoa wa Morogoro,baadhi ya waandishi wa habari na maaskali wa
kike walijikuta wakishindwa kutekeleza majukumu yao na kuangua vilio kwa
uchngu baada ya kuliona jeneza la marehemu Nasra.
Akizungumza na
waandishi wa habari nje ya Mochwari Afisa huyo wa Ustawi wa Jamii
alisema Mwili wa Nasra utaangwa kesho katika Uwanja wa Jamhuri majira ya
saa 2 asubuhi hadi saa 5 asubuhi ambapo baadae utasaliwa kwenye mmoja
wa misikiti ya Manispaa ya Morogoro.
" Baada ya kushwariwa swara ya Adhuhuri tutaelekea makaburi ya Kolla kumuhifadha mepndwa wetu Nasra"alisema Ngungamtitu.
Kama kawa Mtandao huu utakuwepo kwenye matukio hayo hivyo endelea kutembele mtandao huu siku zote
R.I.P Mtoto Nasra
1 comment:
inna lillah waina illahim rajiun Allah amuweke katika watu wema peponi amin.
Pole sana family nzima ya nasra,pamoja na ndugu na jamaa wote wahusika.
Allah akupe moyo wa wakustahamilli wenye subra zitto kwabwe pamoja na family yako yote.
huu ni wakati wa kuwa na moyo wa subra illi muweze kufaulu mitihani ya Allah.
Sisi sote waja ndo njia yetu hii na Allah anatuonyesha mfano kwamba hakuna atakaye baki duniani ile yeye wakati ukifika kila mtu aatakwenda na wakati wake so tutende mema kwa wingi hapa duniani na tutendeane wema kwa kila kiumbe mwenzetu ili watu watukumbuke kwa mema yetu na tuishi na watu kwa wema na tumuogope Allah tusikufuru na kupitiliza na kusahau kwamba hapa duniani tunapita njia tu tuko safarini.
inna lillah waina illahim rajiun Allah amghufiriye na amuweka pema peponi amin amin amin
Post a Comment